Ligi kuu ya Soka la England inatarajia kuendelea tena Wikiendi hii baada ya kupisha michuano ya FA CUP ambapo leo Jumamosi kutakuwa na michezo sita.
Vinara wa ligi Leicester city dhidi ya Norwich city, Southampton na Chelsea, Stoke itaikaribisha Aston Villa, Watford itaivaa Bournemouth, West Brom na Crystal Palace, West Ham itaikaribisha Sunderland.
Jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa michezo miwili Manchester united watakuwa wenyeji wa Arsenal uwanja wa Old Traford, na Tottenham wakiwakaribisha Swansea city, huku michezo miwili ikiaharishwa Liverpool itachuana na Everton,New castlle watakuwa wenyeji wa Manchester city.