Vyungu Hivi ni Zaidi ya Utalii Wilayani Mufindi, Iringa

 Vyungu Hivi ni Zaidi ya Utalii Wilayani Mufindi, Iringa

Vyungu Hivi ni Zaidi ya Utalii Wilayani Mufindi, Iringa

Mmiliki  wa mtandao huu  mzee wa matukiodaima juu akiwa amejitwisha  kichwani  kiatu cha asili  kilichotengenezwa kwa  udongo  ambacho  kinauzwa kati ya Tsh  160,000 kwa  kimoja na  pea moja ni Tsh 320,000 kiatu  hiki ni  moja kati ya  vivutio vya utalii katika  wilaya ya Mufindi  mkoani Iringa vinavyotengenezwa  eneo la Rungemba na kuvutia  watalii  wa ndani na nje
Baadhi ya  vifaa mbali mbali  vilivyotengenezwa kwa udongo  eneo la  Rungemba  Mufindi  ni  zaidi ya  utalii
Majiko  na  vyungu vilivyotengenezwa kwa  udongo
Mmoja kati ya  wanahabari  mkoani Iringa  Mawazo Marembeka akitazama  vyungu eneo la  Rungemba Mufindi mkoani Iringa
Afisa utalii kanda  ya  kusini Tanapa  Bi Risala Kabongo (kushoto)  akitazama  vyungu na  dhana  mbali mbali za  kitalii  eneo la  Rungemba
Kiatu  kilichotengenezwa  kitalii  zaidi kwa udongo
Na  MatukiodaimaBlog
VYUNGU
vya  asili   vinavyotengenezwa  kijiji  cha Rungemba katika  wilaya ya
Mufindi  mkoani  Iringa  vinaweza  kusaidia  kuitangaza  wilaya ya
Mufindi kiutalii  zaidi  iwapo  serikali  ya  wilaya  hiyo
itawawezesha  na  kuwahamasisha  zaidi  wananchi  wilayani  humo
kujiajili wenyewe katika ufinyanzi.
Kijiji
hicho  cha Rungemba ambacho kwa sasa  wananchi  wake hasa wanawake
wameendelea  kujipatia  kipato  zaidi kutokana na ufinyanzi  wa  vyungu
na mapambo  mbali mbali  yatokanayo na ufinyanzi ,kimeendelea  kujipatia
wageni  zaidi  wa ndani na nje  ambao  wamekuwa  wakifika  kupata
huduma  ya  kazi itokanayo na ufinyanzi.
Akizungumza
na mtandao  www.matukiodaima.co.tz mmoja  kati ya  wanawake
wanaojishughulisha na  ufinyanzi  wa  vyungu eneo hilo Bi Anna Kalinga
alisema kuwa awali  walianzisha  eneo  hilo kama  utani  utani  ila
kwa  sasa  eneo  hilo  limeendelea  kupata  umaarufu mkubwa na hata
gharama za  vyungu na  mapambo  mengine  imeendelea kukua zaidi.
Hata
hivyo  alisema  kuwa  idadi ya  wananchi  kupenda  kutengeneza vitu
vya utalii  kwa  kutumia udongo  imeendelea  kuongezeka huku baadhi ya
watu  wameanza  kuboresha maisha  yao kwa  kujenga  nyumba za kisasa na
kusomesha  watoto  kupitia kazi za ubunifu  wa kitalii.
Alisema
katika   eneo hilo  wanatengeneza  vitu  mbali mbali za kitalii
vikiwemo  vitu mfano  wa viatu vya  kupandia maua  ambavyo  gharama
yake ni kati ya 160,000 hadi  320,000  kwa viatu  viwili  kwa maana ya
pea  moja huku  vyungu  vimekuwa  vikiuzwa kati ya  shilingi  45,000
hadi 75,000 na kuwa  bei  hiyo  imepandishwa kutokana na ongezeko  la
watalii katika  eneo hilo .

Eneo   hili kwa  sasa limeendelea  kuwa maarufu  sana  kwa kutangaza
utalii   na utamaduni  wa kitanzania  kupitia ufinyanzi  ila  bado
serikali haijatambua na  kuelekeza  nguvu  zake  zaidi  eneo  hilo kwa
kuweka  utaratibu mzuri  wa kuvutia watalii  kufika  hapa”
Mkuu
wa  wilaya ya  Mufindi  Evarista  Kalalu  akizungumzia  utalii  wa eneo
hilo alisema  wilaya  yake  ilianza mchakato  wa  kubainisha  vivutio
vya utalii pamoja na  kukusudia  kushirikiana na familia ya Chifu
Mwinyigumba  ili  kuweka mazingira mazuri eneo la  makaburi kama  sehemu
ya historia  pindi  watalii  wanapofika  kutembelea   eneo  hilo.
Wakati
kwa upande wa   wasanii  hao  wanaotangaza  wilaya  kupitia  ufinyanzi
za  vitu mbali mbali za  utalii alisema ofisi yake  ilianza mwaka 2007
kwa  kuwapeleka   baadhi ya  wana kikundi  Kyela  mkoani Mbeya
kujifunza namna ya  utengenezaji  wa  vyungu  bora  na dhana  nyingine
ili  kuvutia  watali zaidi  japo kwa  sasa  wilaya  hiyo haina  afisa
utalii baada ya  aliyekuwepo  kufariki  dunia mwaka jana .

Afisa
utalii kanda  ya  kusini Tanapa  Bi Risala Kabongo alisema  kuwa   eneo
hilo la Rungemba ni moja kati ya maeneo ya  vivutio vya  utalii katika
mikoa ya  kusini na kuwa  wilaya ya  Mufindi  pamoja na  vivutio
vingine  bado  wanapaswa  kuboresha  eneo  hilo ili  kulitumia kama
sehemu ya utalii  na kuwa suala la  utalii  linajumhisha mambo mbali
mbali yakiwemo ya hoteli ,biashara  na wanyama  ,maji ,tamaduni ,na
mambo mengine  mengi ambayo wageni  hupenda  kujifunza .