Vyama Vya Siasa, Tumea ya Uchaguzi Wala Kiapo cha Uchaguzi

Vyama Vya Siasa, Tumea ya Uchaguzi Wala Kiapo cha Uchaguzi

Vyama Vya Siasa, Tumea ya Uchaguzi Wala Kiapo cha Uchaguzi


MAADILI YA UCHAGUZI KWA AJILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI YA MWAKA 2015

(chini ya Kifungu cha 124A cha Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya mwaka 1985 (sura ya 343)

SISI Vyama vya Siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pamoja tumekubaliana kuwa na uchaguzi huru, wa haki, uwazi, na wa kuaminika. Na kwamba Amani, Ustawi wa Nchi, Usalama wa Raia, Uhuru wa Vyama vya Siasa na Utii wa Sheria, Kanuni na taratibu za uchaguzi ndio msingi wa uchaguzi ulio huru, haki na wenye kuzingatia ushiriki wa makundi yote ya jamii katika uchaguzi. Tunajipa, na tunakubaliana kuwajibika kuyatekeleza maadili haya yanayotokana na kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 1985, (sura 343). Tutafanya jitihada za wazi kuhakikisha maadili haya yanajulikana na kuheshimiwa na wagombea na wanachama wote wa Vyama vya Siasa.

2.0 Maadili kwa Vyama vya Siasa na Wagombea katika kuendesha shughuli za Siasa wakati wa Kampeni.

2.1 Wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea.

(c) Vyama vya Siasa vifanye mikutano ya Kampeni kwa kuzingatia ratiba rasmi iliyoratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi au Wasimamizi wa Uchaguzi katika kutangaza sera zao. Aidha, mikutano yote itafanyika kati ya saa 2:00 asubuhi na saa 12:00 jioni. Bila kuathiri muda ulioelezwa hapo juu, Vyama vya Siasa vinaweza kutumia vipaza sauti kuanzia saa1:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku kutoa matangazo ya mikutano itakayofuata.

(k) Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea au Wafuasi wao wahakikishe kuwa majengo wanayotumia kufanya kampeni sio ya ibada au sehemu zinazotumiwa kwa ajili ya ibada. Vile vile, Vyama vya Siasa vihakikishe kuwa havitumii Viongozi wa dini kupiga kampeni kwa ajili ya Vyama vya Siasa au Wagombea wao.

(f) Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea wao hawaruhusiwi kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo ya kampeni ya Vyama vingine vya Siasa na matangazo ya Uchaguzi yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.