KUNDI la waandamanaji waliokuwa wakifanya fujo Kaskazini mwa Mji wa London wamechoma moto magari ya polisi na kupora maduka mbalimbali hapo jana, baada ya kuandamana wakipinga kuuawa kwa mtu mmoja aliepigwa risasi na polisi siku ya alhamisi.
Zaidi ya watu 200 walikusanyika karibu na kituo cha polisi cha Tottenham kabla ya maandamano hayo kugeuka kuwa vurugu. Taarifa ya Polisi mjini London imesema, waliwarushia chupa maofisa wa polisi waliokuwa kwenye doria kabla ya kuyachoma moto magari ya polisi na basi moja.
Alhamisi iliyopita, katika tukio moja la kufyatuliana risasi na polisi, lilisababisha kifo cha mwanaume (29). Polisi wanasema bado uchunguzi unafanywa kuhusiana na tukio la mtu huyo.