1) Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans akifafanua jambo kwa mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin wakati wakielekea kweye wodi ya wagonjwa wa Fistula inayofadhiliwa na Kampuni y a simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
2) Muuguzi wa Hospitali ya CCBRT kitengo cha wagonjwa wa Fistula Bi. Emelda Lweno akitoa maelezo kuhusiana na jinsi wanavyowahudumia wagonjwa wa Fistula kwa mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin wakati alipozuru katika wodi hiyo hospitalini hapo.
3) Muuguzi wa Hospitali ya CCBRT kitengo cha wagonjwa wa Fistula Bi. Emelda Lweno akimwonesha mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza , Elizabeth Filkin wanawake wenye ugonjwa wa Fistula ambao matibabu yake yanafadhiliwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania wakati wa ziara yake hospitalini hapo.
4) Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans akimpatia maelezo Mjumbewa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Huduma kwa Jamii wa Vodafone ya nchini Uingereza Bi Elizabeth Filkin wakiwa katika wodi ya wagonjwa wa mdomo sungura alipotembelea hospitalini hapo kuona maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Vodacom Foundation. Kulia ni Mkuu Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimjulia hali mtoto mwenye tatizo la mdomo sungura. Bi Elizabeth yupo nchini kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na Vodacom.
5) Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans akiagana na mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin mara baada ya ziara Hospitalini hapo, watatu kulia ni Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba aliembatana na ujumbe huo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Bi. Haika Mawalla.