Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini, Halima Omary Dendego (kushoto)akishuhudia Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh akimkabidhi madafutari Zainabu Omary ambae ni mtoto anaeishi katika mazingira magumu mkoani Tanga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ramadhan Care & Share iliyozinduliwa mjini humo ikiwa na lengo la kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 sehemu mbalimbali nchini wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, katikati ni Mkuu wa wa Kampeni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini wapili toka kushoto, Halima Omary Dendego akikabidhi mbuzi pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, kwa watoto yatima wa mkoani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inayolenga kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 sehemu mbalimbali nchini wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Kampeni hiyo inaendeshwa na Vodacom Foundation.
Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu wakiwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Tanga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ramadhan Care & Share iliyozinduliwa mkoani humo ikiwa na lengo la kufuturisha watoto zaidi ya 500 sehemu mbalimbali nchini wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.