Mtoto yatima wa kituo cha T.H.M.H cha Magomeni jijini Dar es Salaam, Rebeca Elias akiwa ameshikilia mbuzi mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Stela Chiwango aliemshika begani na Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba (watatu kulia) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya Krismas, Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya milioni 50 katika kampeni hiyo, wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hiyo kitengo cha huduma kwa wateja.
Mkuu wa Kitengo cha Kusaidia Jamii cha Vodacom Tanzania 'Vodacom Foundation', Yessaya Mwakifulefule akitwishwa kiroba cha Maharage na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu kushoto na Meneja wa akaunti na usajili wa namba za simu Loius Maro,wakati wa kupakua mizigo hiyo tayari kwa kuwagawia msaada vituo mbalimbali vya watoto yatima jijini Dares salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja tayari kuelekea katika vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dares Salaam mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Share and Care hapo jana ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya milioni 50 katika kampeni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakicheza pamoja na watoto yatima wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care hapo jana ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya milioni 50 katika kampeni hiyo.