Vodacom yawatembelea wateja wake kujua changamoto

Msafara wa magari ya Vodacom Tanzania ukipita katika barabara ya Morogoro maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam yakiwabeba wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa kuazimisha siku ya wateja ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo walienda mitaani kuelimisha wateja kuhusu huduma ya M-Pesa na promosheni zinazoendelea za punguzo la utumaji fedha la asilimia 75 na bonasi hadi asilimia 25 unaponunua muda wa hewani kupitia M-Pesa.


Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakibandika matangazo katika moja ya kibanda cha duka Mbagala Zakiemu yakionesha huduma za M-Pesa wakati wafanyakazi hao walipokuwa wakiazimisha siku ya wateja ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo walienda mitaani kuelimisha wateja kuhusu huduma ya m-pesa na promosheni zinazoendelea za punguzo la utumaji fedha la asilimia 75 na bonasi hadi asilimia 25 unaponunua muda wa hewani kupitia M-Pesa.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom imeanza kuwatembelea wateja wao nchi nzima ili kujua changamoto ambazo wanakutana nazo baada ya kuzindua promosheni ya punguzo la huduma ya kutuma pesa (M-Pesa) kwa asilimia 75. Zoezi hilo ni pamoja na kujua changamoto za huduma hiyo na namna ilivyopokelewa kwa wateja wake na kupokea maoni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza alisema kwa kutambua umuhimu wa wateja wao hapa nchini kampuni hiyo imetenga siku muhimu ijulikanayo kama ‘Siku ya masoko’ ili kuangalia jinsi gani wateja wao walivyo elewa na kuzipokea huduma zao.

“Wafanya kazi wote wa Vodacom nchi nzima wakiongozwa na wakurugenzi na washiriki wote wa kampuni yetu watawatembelea mawakala na wananchi ili tuangalie changamoto gani wanazokutana nazo na kusikiliza ushauri wao.

“Tatizo la mawasilianio ni kubwa sana tumekuwa tukipata malalamiko kutoka kwa wateja wetu hivyo kwa kutumia siku hii muhimu tutajua matatizo yote ambayo wateja wetu wanakutana nayo,” alisema Meza.

Naye Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom, Mwamvita Makamba alisema huduma ya M-Pesa imerahisisha maisha kwa wananchi wa hali zote nchini kwani kwa kutumia huduma hiyo wateja wameweza kulipia huduma ya Luku pamoja na ada kwa wanafunzi bila matatizo.

Kampuni ya Vodacom imeweka kianzio cha Sh. 50 cha kutuma pesa na bonasi ya asilimia 25 kwa wateja wake ambayo itaenda sambamba na zawadi ya kitita cha Sh. milion 480 kushindaniwa. Maeneo ambayo yametembelea na Vodacom kwa Jiji la Dar es Salaam ni pamoja na Kariakoo, Tegeta, Kimara, Mbezi pamoja na Mbagala.