Vodacom yawakopesha akinamama mil 30 kupitia mradi wa MWEI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akimkabidhi fedha, Mwanaidi Said ambaye ni mmoja wa akinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga cha Mlandizi mkoani Pwani, fedha hizo zilitolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa MWEI kwa ajili ya kusaidia wakinamama wajasiliamali na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya m-pesa bila riba. Jumla ya kinamama 425 walinufaika na mkopo huo wenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 30. Katikati ni Meneja mradi huo, Mwamvua Mlangwa.

Meneja wa Mradi wa MWEI unaondeshwa na Vodacom Tanzania, Mwamvua Mlangwa, akimkabidhi fedha, Radhia Abdalah ambazo ni mkopo usio na riba inayotolewa na kampuni hiyo na kurudishwa kwa njia ya m-pesa, zaidi ya sh. milioni 30 zimetolewa kwa vikundi vya kinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga kilichopo Mlandizi mkoani Pwani, Jumla ya kinamama 425 wamenufaika na mkopo huo

Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule akifafanua jambo kwa wakina mama wajasiliamali wa Mlandizi mkoani Pwani, kuhusiana na matumizi ya mikopo waliyopewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wa MWEI, Vodacom kupitia mradi huo umewanufaisha jumla ya wanawake 425 kwa kuwapa mikopo isiyo na riba wa zaidi ya sh. milioni 30 mkoani Pwani.