Vodacom yatoa semina kwa taasisi za fedha juu ya huduma ya M-Pesa

Washiriki wa semina ya Taasisi za kifedha (TAMFI) wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha Vodacom M-Pesa, Franklin Bagalla wakati wa semina hiyo mahususi kwa ajili ya taasisi hizo kunufaika na huduma ya Vodacom M-Pesa, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha Vodacom M-Pesa, Franklin Bagalla na Meneja wa Vodacom M-Pesa, Magesa Wandwi wakisikiliza swali kutoka kwa mratibu wa Taasisi za Kifedha wa Mkoa wa Arusha, Hamisi Shelukamba wakati wa semina ya Taasisi za kifedha (TAMFI) iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya kunufaika na huduma ya M-Pesa, semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam.