
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha Polisi Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967, kwa gharama ya sh. milioni 17. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, jumla ya sh. milioni 17 zilitumika katika kukarabati kituo hicho. Kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye kushoto akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando kulia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba akishuhudia, jumla ya sh. milioni 17. zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha sh. milioni 17, wakishuhudia ni Mkuu wa Kituo hicho INSP Amilton Matagi, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando.