Vodacom yadhamini mashindano ya uvuvi Kisiwani Sinda

Commodore Spiras Manoloudis wa Yatch Club jijni Dar es Salaam (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa wadhamini wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda hivi karibuni ambao ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, (kulia) Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza.

Washindi wa mashindano ya uvuvi ya Latham Open wakifurahia tuzo zao za ushindi mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika Kisiwani Sinda mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

Wafanyakazi wa Boti ya Mistress wakiwa wamebeba samaki zilizovuliwa katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi yajulikanayo kama Latham Open yaliyoshirikisha nchi sita na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.