Vodacom kudhamini maonyesho 36 ya Sabasaba

Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kulia) akimuonesha Afisa Udhamini na Matukio wa Kampuni hiyo Ibrahim Kaude,simu ya mkononi aina ya ZTE s502 yenye Radio na Michezo inayouzwa kwa Tsh 13,000 ikiwa na muda wa maongezi ya Tsh 6,000 ukitaka kupata simu hizo fika katika mabanda ya Vodacom yaliyopo katika viwanja vya maonesho ya 36 ya Biashara Kimataifa(Sabasaba)

[caption id="attachment_19443" align="aligncenter" width="569"] Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiandaa mabanda katika viwanja vya maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam,ambapo wateja watajipatia huduma mbalimbali pamoja na simu ya mkononi aina ya ZTE s502 yenye Radio na Michezo inayouzwa kwa Tsh 13,000 ikiwa pamoja na muda wa maongezi ya Tsh 6,000

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania mwaka huu ni wadhamini Wakuu ambao wataratibu habari na Mawasiliano katika Maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, hivyo wananchi wote wanatangaziwa kufika katika Viwanja vya maonesho hayo,kujione na kupata huduma bora katika viwanja hivyo.