Vita dhidi ya saratani ya matiti ni yetu sote

timu hii ndiyo iliyoiwakilisha Tanzania

NI MFANO mzuri wa kuigwa nchini Tanzania kama kujali na kuwapa moyo kina mama walioathirika na saratani ya maziwa kwani pia wanahitaji kuthaminiwa, kutoa elimu ya kujikinga pamoja na wale walioathirika na ugonjwa huo, ili kupata changamoto za kwenda kupima kila mwenzi, kwani ni ugonjwa hatari unao waumiza sana kina Mama wa Mijini na Vijijini huko nyumbani.
Tungeliomba makampuni makubwa kufikiria zaidi na kuwasiliana na kiongozi mzima wa Team Tanzania ambao wanauzowefu mkubwa katika Susan G. Komen Global Race for Care, wanaweza kukupeni mawazo zaidi juu ya kutoa msaada huo kwa kina mama walioathirika, wale familia zao tayari wameshakubwa na ugonjwa huo wa Saratani ya Maziwa.

Ili kutoa mifano kwa wengine ambao bado wanahitaji mafundisho ya kujikinga na ungojwa huo, kwa mwendo huo wa mkosanyiko wa watu ambao utaleta muamko mkubwa na elimu kwa waTanzania wote, na kujisikia tupo katika muamko flani dhidi ya kutokomeza ugonjwa huu hatari unao wakumba kina Mama wote Duniani.

Vile vile Team Tanzania imetoa shukurani kwa waTanzania wote walioshiriki katika matembezi ya “Susan G. Komen Global Race for the Cure”, pamoja na wale ambao hawakuweza kushirikiana nao kwa michango yao mbali mbali katika kufanikisha shughuli hii.

Pia walitoa shukurani kubwa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani kwa ushirikiano wao uliotoa kuweza kufanikisha shughuli hiyo, pia kutoa shukurani kwa vyombo vya mawasiliano katika Jumuia ya Watanzania kwa mchango wao mikubwa wa kutawanya habari hizo.

Ni wajibu wetu kufikisha habari hizi nyumbani ili iwe kama zawadi ya mafundisho ya kile tulichokichuma ugenini kukileta nyumbani, ili waathirika wa ugonjwa huu hatari tuweze kuutokomeza kwa hali na mali, kuwa kitu kimoja kama waTanzania tunaojali na kuthamini nchi yetu, kwani kitaifa tunaweza.