Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea Banda la TTCL katika maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Kibiashara katika viwanja vya Sabasaba. Mama Salma katika mazungumzo yake aliipongeza TTCL kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuleta maendeleo nchini.
Baadhi ya wateja wa TTCL na wananchi wengine wakitembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba.
Viongozi Waipongeza TTCL Maonesho ya Sabasaba

VIONGOZI mbalimbali wa Serikali waliotembelea Banda la Kampuni ya TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba wameipongeza kampuni hiyo kwa utendaji kazi.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Mlengeya Kamani alimwaga pongezi hizo kwa TTCL alipotembelea banda hilo, ambapo aliipongeza Kampuni ya Simu TTCL kwa kazi nzuri ya kusimamia mawasiliano nchini. Kwa upande wake mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akitembelea banda la TTCL alipongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia sekta ya mawasiliano.
Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL ambayo pia katika maonesho hayo imefanikiwa kushinda tuzo katika kundi la kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano, inashiriki katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Banda la TTCL limeendelea kuwa kivutio katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea ambapo wananchi wamekuwa wakifurika katika banda hilo kushuhudia bidhaa na huduma anuai zilizoletwa kwenye maonesho hayo.