Viongozi wa ECOWAS wasitisha safari Mali

UJUMBE wa viongozi wa Afrika Magharibi umeachana na mpango wake wa kwenda Mali kujadiliana na viongozi wa mapinduzi ya wiki iliyopita. Taarifa zinasema kwa sasa viongozi hao wataendesha mazungumzo hayo mjini Abidjan.

Taarifa zaidi zinasema uamuzi huo umekuja baada ya maandamano ya watu wanaounga mkono mapinduzi kuvamia uwanja wa ndege katika eneo la kupaa na kutua ndege ili kupinga ujio wa viongozi hao.

Nchi jirani na Mali tayari zimeshatamka kuunga mkono mapinduzi hayo ya Mali kukaa pembeni. Zimeweka majeshi ya kulinda amani katika tahadhari tayari.
Jumatano maelfu ya watu waliandamana mitaani kuunga mkono mapinduzi hayo.

Wengi walikasirishwa na kile wanachokiita kuwa ni ‘kuingiliwa mambo ya ndani na wageni’

“Viongozi wa mapinduzi wanatakiwa kutatua matatizo kaskazini,ufisadi na elimu. Hayo ni muhimu kuliko uchaguzi. “Mmoja wa waandamanaji, Khalifa Sogo, aliwaambia waandishi wa habari.

Viongozi wa mapinduzi wametoa maelezo ya katiba mpya pamoja na kutangaza tarehe ya uchaguzi ambapo wale waliohusika na mapinduzi hawataruhusiwa kushiriki ingawa tarehe halisi haijatangazwa bado.

Mapinduzi yaliongozwa na askari ambao hawakufurahishwa na jinsi serikali ya Bw Toure ilivyokuwa ikishughulikia suala la waasi wa Tuareg kaskazini mwa nchi. Waasi wa Tuareg wameliviondoa vikosi vya jeshi katika miji kadhaa ya kaskazini katika miezi ya hivi karibuni.

Chini ya katiba mpya kamati ya mpito yenye wajumbe 26 kutoka vikosi vya usalama na raia 15 watashirika madaraka. Wale watakaofanya kazi katika kamati hiyo wamepewa kinga ya kushtakiwa. Baadhi ya nyaraka katika katiba hiyo zinafanana na katiba ya sasa yaMalizikiwemo uhuru wa kujieleza, mawazo na kutembea.
-BBC