KAULI ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama ya kuwataka viongozi wa serikali za vijiji kuondoka katika ofisi walizokua wakizitumia awali na kwenda kupanga majengo ya watu binafsi imepingwa vikali na wananchi pamoja na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kauli ya Mkuu wa mkoa aliitoa Februari 5, 2015 wakati alipokua akizungumza na viongozi wa kata, vijiji na vitongoji katika Ukumbi wa shule ya sekondari ya Shauritanga iliyopo wilayani Rombo kufuati malalmiko a muda mrefuaviongozi wa cadema wa vijiji kulamikia viongozi wa zamani wa CCM kugoma kukabidhi ofisi hizo ambazo wanadai zimejengwa kwa michango ya wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa ofisi hizo ni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivyo viongozi hao wanatakiwa kuhama katika ofisi hizo na kupanga nyumba za watu binafsi kwa gharama ya serikali.
Baada ya kikao hicho ambapo hawakupewa fursa ya kuuliza maswali Viongozi hao nje ya Ukumbi huo walikusanyikana kpinga kauli hiyo ambapo wamesema kuwa watasimamia na kulinda maliza wananchi na kuwa hawapo tayari kuonamali zawananchi zinaporwa.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi, Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasin alisema amesikia malalmiko ya wananchi na kwa sasa anafanya utaratibu wa kufikisha malalamiko hayo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.