Mbunge Mgimwa akizungumza na wananchi wake baada ya kupokea wana chama wa Chadema
Na MatukiodaimaBlog
VIONGOZI watatu wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi (UKAWA) Kata ya Lyamgungwe Jimbo la Kalenga wamempongeza mbunge wa jimbo la hilo, Godfrey Mgimwa kwa kutekeleza ahadi mbalimbali zilizoachwa na marehemu mbunge aliyepita Dk. Wiliam Mgimwa kwa muda mfupi na kuwa katika kuonyesha umoja wao wameamua kuunganisha nguvu zao kwa
mbunge huyo kwa kuhama Chadema na kujiunga na CCM.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzao zaidi ya 20 ambao walikuwa nyuma yao kabla ya kujiengua Chadema na kujinga na CCM walisema kuwa sababu ya kujiunga na upinzani ilitokana na makundi ndani ya CCM na upendeleo wa uteuzi wa wagombea mbalimbali pamoja na wabunge waliotangulia kuonyesha kutumia ubunge kulea familia zao badala ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo jambo ambalo mbunge Mgimwa amekuwa wa tofauti na wabunge wengine kwa kuonyesha kuwajali zaidi wapiga kura wake.
Bw. Mapinduzi Kalolo ambae alikuwa ni viongozi wenzake wengine
waliorudi CCM ni pamoja na katibu kata, mwenyekiti na wajumbe na kuwa kujiunga kwao Chadema ni baada ya mambo ndani ya CCM kutokwenda vizuri ila kwa sasa mbunge wao ameendelea kuwaunganisha wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.
Pia alisema walipotoka CCM kwenda Chadema walikuwa wameahidiwa mambo mengi na viongozi wa Chadema jimbo hilo la Kalenga ila baada ya kujiunga utekelezaji wa ahadi walizotoa ikiwemo ya kufungua ofisi
ilionekana na ngumu na kuwa chama hicho hata kuwajali kilishindwa na
hivyo kuishia kuonekana si chochote katika kata hiyo zaidi ya
kutumika kama karai na Chadema.
“Kujiunga na Chadema kweli tulikuwa tumepotea ila kwa sasa tumeona ni vema kurudi kwa baba na mama CCM baaba ya maisha ya kuishi kama mwana mpotevu kutushinda…hivyo tunakuhakikishia mheshimiwa mbunge Mgimwa wewe ndio umetushawishi kuhama Chadema na kujiunga na CCM kutokana na kuonyesha mfano katika kutekeleza ahadi zao kwa wananchi…kalenga hatujapata kuwa na mbunge ambae amefanya mambo makubwa kama wewe ndani ya miezi minne …haya uliyofanya wewe wabunge wengine walikuwa wakishindwa kuyafanya kwa kipindi cha miaka 5 ya ubunge.”
Hata
hivyo Kalolo alisema kuwa ni matumaini makubwa kwao kuwa kazi
iliyofanywa na mbunge Mgimwa kwa kipindi kifupi cha miezi minne
ama cha mwaka mmoja wa utawala wake ni imani tosha kwao kwa
kuendelea kumchagua zaidi kwa miaka mingine 10 mbele ili
kuliwezesha jimbo hilo kuwa la mfano zaidi.
HIvyo
alikitaka CCM kuacha tabia ya viongozi wake wa wilaya kuwaruhusu
baadhi ya wana CCM kuzunguka kuwavuruga wapiga kura kwa kubeza
jitihada zinazofanywa na mbunge Mgimwa na kuwa kufanya hivyo ni
kukaribisha upinzani katika jimbo hilo.
Kalolo
alisema iwapo viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa watashikamana
na mbunge Mgimwa upo uwezekano wa upinzani kufutwa kabisa katika
jimbo hilo ambalo halijapata kuwa na historia ya kuongozwa na
upinzani.
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa Jimbo la Kalenga kupitia
Chadema Dk. Salum Kalolo alisema kuwa kuondoka kwa viongozi hao
Chadema na kujiunga na CCM kutokana na utendaji wa mbunge huyo
Mgimwa hawajakosea kwani kwa mtazamo wake kazi inayofanywa na mbunge huyo jimboni inapaswa kuungwa mkono na kila mwananchi bila kujali itikadi ya chama chake.“
Wengi walijua kuwa kutokana na ujana wake mambo ya maendeleo
yasingeweza kusonga mbele ila mimi si CCM mimi ni Chadema kutoka
sakafu ya moyo wangu ninampongeza munge Mgimwa amekuwa mbunge wa mfano katika kutuletea maendeleo Kalenga,”
Zipo
changamoto mbali mbali ambazo iwapo atapewa muda wake wa kipindi
japo kimoja cha miaka 5 kuanzia mwakani 2015 tungependa atusaidie
kutatua ni pamoja na adha ya maji na uboreshaji wa shule za msingi
ambazo nyingi hazipo katika hali nzuri.
Hata
hivyo mbunge Mgimwa alisema malengo yake ni kuweka rekodi nzuri ya
ubunge katika jimbo hilo la Kalenga na kulifanya kuwa jimbo lenye
maendeleo makubwa ikiwa ni pamoja na kuona ndoto yake ya kuanzisha
benki ya wananchi wa Kalenga inaanzishwa ili kusaidia kuwakopesha
wakulima mitaji.
Kuhusu
suala la maji alisema tayari katika baadhi ya maeneo ameanza
kutekeleza ahadi ya maji safi pamoja na kupeleka umeme katika kata ya
Mgama na Magulilwa ili kuchochea kasi ya maendeleo japo maombi yake
kwa wananchi ni kuendelea kumwombea zaidi ili ndoto yake ya kuleta
maendeleo ifanikiwe zaidi.
|