Viongozi Somalia wapitisha Katiba Mpya

Wananchi wa Somalia

VIONGOZI nchini Somalia wanaokutana Mjini Mogadishu kwa wingi wameipitisha Katiba Mpya ya nchi hiyo kitendo ambacho kimefungua njia kwa Serikali mpya kuchaguliwa mwezi huu.

Kura hiyo imepigwa muda mfupi baada ya watu wawili kujilipua wenyewe nje ya jingo la mkutano. Chini ya mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa bunge jipya litachagua kiongozi mpya wa Somalia Agosti 20.

Somalia imekuwa katika vita na kundi la al-Shabab kwa miongo miwili na huku kundi hilo likidhibiti maeneo mengi ya nchi. Serikali yake ya mwisho iliondolewa madarakani mwaka 1991.