Viongozi Somalia wakubaliana

Viongozi Somalia katika makubaliano

VIONGOZI wa Somalia wametia saini mkataba ambao wanataraji utamaliza mvutano na mgogoro uliopo katika nchi hiyo. Katika makubaliano hayo wameridhia kuwepo kwa Bunge jipya pamoja na baraza la pili la wazee na Serikali za Majimbo.

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini na Serikali ya sasa, utawala wa majimbo mawili, na wanamgambo wanaounga mkono Serikali, yatajadiliwa juma lijalo, kwenye mkutano wa London kuhusu Somalia.

Lakini kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab, ambalo linadhibiti sehemu kubwa ya kati na kusini mwa nchi hiyo, hawakushiriki kwenye makubaliano hayo.
-BBC