Viongozi Maarufu 40 Afrika Washiriki Sherehe za Muungano Tanzania…!

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano. Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano. Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam

ZAIDI ya viongozi maarufu 40 kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika na nje ya bara la Afrika wakiwemo marais na makamo wa marais, marais wastaafu, wafalme, mawaziri, mabalozi, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na viongozi wengine lukuki wameshiriki katika maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliozaa nchi ya Tanzania.

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein kwa pamoja na viongozi wa juu wa pande zote za Muungano wa Tanzania leo wamewaongoza wageni hao maarufu kusherehekea miaka hiyo 50 ya Muungano iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.

Sherehe hizo ambazo zilitawaliwa na mbwembwe za hali ya juu ambazo zilikuwa kivutio zaidi kwa Watanzania pamoja na viongozi wa mataifa anuai na wageni maarufu kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika zilianza majira ya saa tatu asubuhi na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi ambao wengine walikosa eneo la kukaa hivyo kuruhusiwa kukaa pembezoni mwa uwanja wa Taifa eneo ambalo waliweza kushuhudia matukio moja kwa moja kwa mbali.

Marais wa mataifa manne wameshiriki katika sherehe hizo, yaani Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Burundi, Piere Nkurunzinza, na Rais wa Malawi, Bi. Joyce Banda. Wakuu wa nchi wengine ni pamoja na Mfalme wa Lethoto, Mfalme wa Swaziland, Makamu Rais wa Nigeria, pamoja na Makamu Rais wa Zambia.

Wawakilishi wengine waliotumwa na wakuu wa nchi zao kuwawakilisha wakuu wa nchi zao ni pamoja na mawaziri wa Misri, Mozambique, Rwanda, Zimbambwe, Comoro, Usheliusheli, Oman, Ethiopia, Sudan Kusini, Angola na Algeria. Nchi zilizowakilishwa na mabalozi ni pamoja na Kuwait, Mauritius, Botswana, Ghana, Ufaransa, Korea Kusini, Brazil, Uholanzi, Finland, Uingereza, Elitrea na taifa la Qatar.

Viongozi wengine na wakuu wa taasisi za kimataifa waliohudhuria sherehe hizo pia ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Spika wa Bunge la Congo, DRC, marais wastaafu wa Namibia, Zambia, Kenya na Tanzania yenyewe, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara China na viongozi wengine wengi waalikwa.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Baadhi ya Mawaziri wa Tanzania Bara na Visiwani, Viongozi wa vyama na Serikali, viongozi wa taasisi za serikali na zisizo za serikali, wakuu wa idara mbaimbali na viongozi maalufu, wastaafu na wageni anuai walishiriki pia katika hafla hiyo kubwa iliyofana.

Tofauti na maadhimisho ya sherehe za muungano ya nyuma safari hii mbwembwe anuai ziliongezeka hali iliyoleta mvuto zaidi kwa waliokuwa wakishuhudia sherehe za maadhimisho. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ndiyo lililoongeza manjonjo zaidi yaliyokuwa kivutio kwa kila mmoja ambapo makomando maalumu wa kuruka kwenye ndege waliruka na kutua kwenye Uwanja wa Uhuru kwa kutumia miamvuli.

JWTZ pia walionesha kwa washiriki baadhi ya vifaa vya kijeshi vya kisasa ambavyo hutumika katika shughuli zao anuai za utekelezaji majukumu yao, ndege za kisasa za kivita, vifaru, magari yaliyobeba mizinga yalipita mbele ya mgeni rasmi na kutoa heshima za utii. Michezo ya vijana wa alaiki, ngoma, nyimbo, sarakasi na maandamano maalumu yalipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikwete na kutoa heshima.

Sherehe hizo zilianza kwa mkesha uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa pande zote za muungano yaani Zanzibar na Tanzania Bara.