BAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuwashikilia viongozi wawili wa CHADEMA akiwemo aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema, Gervas Mgonja kwa wiki moja kwa tuhuma za kukutwa na silaha na kushiriki matukio kadhaa ya uhalifu wa kutumia silaha leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu madai yanayowakabili.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Ibrahim Kilongo alisema kuwa watuhumiwa hao walitakiwa kufikishwa mahakamani hapo jana lakini ilishindikana kutokana na hati ya mashitaka kushindwa kukamilika.
Alisema watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na walishikiliwa kwa muda mrefu kutokana na uchunguzi wa tuhuma zao pamoja na kufuatilia watuhumiwa wengine wanaopaswa kuunganishwa katika shitaka hilo ili wote kwa pamoja kufikishwa mahakamani.
“Watuhumiwa hao tulitarajia kuwafikisha mahakamani leo asubuhi ikashindikana na mchana pia ikashindikaa lakini kesho asubuhi tutawafikisha ili wasomewe mashitaka yaoā€¯alisema Kamanda.
Aidha mtuhumiwa mwingine katika shitaka hilo ni Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA 9BAVICHA), Anold Kamdye ambao wote walikamatwa juma moja lililopita kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya ujambazi.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chadema wilaya ya Arusha, Kombe akizungumza alisema taarifa walizo nazo kama chama ni kwamba viongozi wao hao walihusika na matukio hayo ya ujambazi na jana mchana watakuwa na kikao ili kujadili suala hilo.
Hata hivyo kiongozi huyo alikutana na vyombo vya habari na keleza kusikitishwa kwao na tuhuma zinazowakabili viongozi wao hao na kusema kuwa chama hakihusiki na tuhuma hizo wala hakikuwatuma na kudai kuwa watuhumiwa hao wakipatikana na hatia chama kitachukua hatua kali za kinidhamu.