Vikundi vya wanawake WAMA vyapewa semina

Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).

Tabu Likoko Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA) akifungua rasmi semina ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa vinavyosimamiwa na Taasisi ya (WAMA) kuhusu huduma za Mfuko wa Bima wa Afya NHIF inayofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA asubuhi hii jijini Dar es Salaam kutoka kulia pichani ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF), Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti na Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji.

Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF) akizungumza katika semina hiyo jinsi mfuko huo unavyosaidia jamii kupata matibabu, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) na katikati ni Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti.