Vijana Kuongezeka Katika Biashara ya Mali Zisizohamishika-Lamudi Tanzania

Timu ya Lamudi Tanzania.

Timu ya Lamudi Tanzania.


BIASHARA ya ununuzi na ukodishaji wa nyumba inashamiri kwa haraka na biashara hii inatumiwa na vijana wengi katika sekta ya uwekezaji hasa miaka ya karibuni. Kwa sasa imefikia asilimia 59.37 ya vijana wenye umri kati ya 25-34, ambao wanajihusisha na shughuli hii, kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na Lamudi, Inaonyesha kuwa watu wengi zaidi wanania ya kuanza biashara hii wakiwa bado vijana.

Utafiti huo, unaonyesha kuwa ukilinganisha vijana wenye umri kuanzia miaka 35-44 katika biashara ya mali zisizohamishika hapa nchini bado kuna kundi kubwa la vijana wanaojihusisha na biashara hii kuanzia umri wa miaka 25 -34. Pia takriban asilimia 35 ya watu wanaotafuta nyumba na wawekezaji ni vijana katika umri huo huo.

“Vijana ndio watu wanaoaminika na wanaoweza kufanya mabadiliko katika sekta hii” Meneja wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa alifafanua juu ya jambo hili. Hata hivyo, ni dhahiri kuwa kuna hatari ya kuwahusisha watu ambao ni wawekezaji wa mali hapa Tanzania hasa ikiwa vijana ambao ni wawekezaji hawajui nini maana ya uwekezaji na hawana elimu yoyote kuhusiana na biashara hii.

“Ili nchi hii iweze kuendelea, tunatakiwa kujihusisha kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. Pia kuna uhitaji wa kutoa mafunzo kwa vijana kuhusiana na biashara ya mali isiyo hamishika ikiwemo nyumba na viwanja ili wawezee kukabiliana na soko la hili”. Godlove aliongeza.

Mapema ndani ya mwaka 2007, serikali ya Tanzania ilitoa Sera ya Vijana Kitaifa. Lendo kuu ni kuboresha hali ya uvivu wa usimamizi wa shughuli za kujenga taifa, vile vile kuwezesha mipango ya maendeleo ya kiuchumi kwa vijana mbali mbali kwa kuwahusisha kushiriki katika sekta tofauti za kimaendeleo ikiwemo ya mali zisizohamishika.

KUHUSU LAMUDI
Ilizinduliwa 2013, Lamudi ni ya kimataifa inayolenga masoko ya juu ya mali zisizohamishika yanayoibukia kwa haraka – Lamudi inaongezeka kwa sasa inapatikana katika nchi 28 katika Asia, Mashariki ya Kati, Afrika na Amerika ya Kusini, na pia ina idadi ya mali zisizohamishika takribani 600,000 kupitia mtandao wake wa kimataifa. Lamudi ni moja kati ya kampuni zinazoongoza na bora, kutokana na kutoa huduma kwa wauzaji, wanunuzi, wamiliki wa ardhi na wakulima ambapo tovuti hii imekuwa ni salama na rahisi kutumia kupata makazi kupitia online.