Van Gaal Kujiuzulu Manchester United Wiki Hii

2453312
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kuwa anaweza “kujiuzulu mwenyewe” baada ya Stoke City kuwapiga magoli 2-0 katika kichapo chao cha nne mfululizo katika michuano yote.

Mholanzi huyo, ambaye anakabiliwa na shinikizo baada ya kucheza mechi saba sasa bila ushindi, aliulizwa katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya mechi iwapo ”anahofia kibarua chake kitaota nyasi?

Kocha huyo mwenye umri wa miaka, 64, alijibu kuwa hjilo lilikuwa jambo analostahili kujibu katika mazungumzo na mkurugenzi wa klabu hiyo Ed Woodward na si vyombo vya habari.

United imekuwa na msururu wa matokeo duni uliosababisha wakatupwa nje ya Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi mbali na kuporomoka kutoka kwenye orodha ya nne bora katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.
daily-star-backpage-28122015_yk0n6s4935jh1af9nxzc60ykx
Van Gaal, aliyechukua nafasi ya David Moyes katika msimu wa 2014, alisema klabu hiyo alimuunga mkono siku zote ila aliongeza:
Hata hivyo mashabiki wataudhika lakini hiyo inatarajiwa baada ya kushindwa mara nne .