Manchester United watakutana na mahasimu wao wa jadi Liverpool katika hatua ya 16 bora katika Europa Ligi.
Tottenham wamepewa miamba wa ligi y Ujerumani Borussia Dortmund baada ya droo kufanywa jana.
Valencia, walio chini ya Gary Neville, watakutana na wapinzani wao katika La Liga Athletic Bilbao.
Sevilla, walioshinda kombe hilo miaka miwili iliyopita, wataanza ugenini dhidi ya Basel katika uwanja wa St Jakob-Park, ambao pia utaandaa fainali.
Mechi hizo zitachezwa Alhamisi tarehe 10 na 17 Machi.Washindi wa ligi hiyo watafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka ujao.
United, ambao hawajawahi kushinda Europa Ligi waliilaza FC Midtjylland kwa jumla ya mabao 6-3.
Marcus Rashford alifunga mabao mawili mechi yake ya kwanza kabisa kuwachezea mechi ya marudiano ambayo United walishinda 5-1 usiku wa Alhamisi.
Liverpool chini ya Jurgen Klopp walisonga kwa kulaza Augsburg 1-0 kwa jumla, bao la pekee likifungwa na James Milner Alhamisi.
Klabu hiyo ilishinda kombe la zamani lililokuwa likijulikana kama Kombe la Uefa mara tatu 1973, 1976 na 2001.
Itakuwa mara ya kwanza kwa United na Liverpool kukutana ligi ya Ulaya.
Droo kamili ya Europa League hatua ya 16
• Shakhtar Donetsk v Anderlecht
• Basel v Sevilla
• Villarreal v B
• ayer Leverkusen
• Athletic Bilbao v Valencia
• Liverpool v Manchester United
• Sparta Prague v Lazio
• Borussia Dortmund v Tottenham
• Fenerbahce v Braga