Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil pamoja na Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi inayotengeneza vifaa vya kuzimia moto vyenye teknolojia ya kisasa vinavyoitwa DSPA 5, wakikiandaa kifaa hicho kwa ajili ya kukirusha ndani ya kontena lililowashwa moto, ili kufunga mlango na kuruhusu kifaa hicho kufungua gesi ya Oxgen baada ya sekunde sita tayari kuzima moto huo ndani ya kontena hilo, tukio hilo lilikuwa ni uzinduzi wa vifaa hivyo hapa nchini, uliofanyika katika viwanja vya Kikosi cha kuzima moto Fire jijini Dar es Salaam leo.
Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi akiwaelezea wageni waalikwa mbalimbali teknolojia ya kisasa ya vifaa vipya aina ya DSPA 5, vyenye uwezo wa kuzima moto kitaalamu kwa waandishi wa habari jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil pamoja na viongozi wa kampuni hiyo na wakuu wa kikosi cha kuzima moto wakishuhudia moshi mkubwa ukitoka kwenye kontena hilo baada ya kifaa hicho kuanza kazi yake ya kuzima moto.
Askari wa Kikosi cha kuzima moto wakiwa tayari kwa kuimza masalia madogo madogo ya moto baada ya kifaa hicho kufanya kazi yake kikamilifu.