Na Robert Okanda
MAKAMPUNI ya kiwango cha kati yanatimiza jukumu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Kwa kutambua hilo, KPMG na Mwananchi Communications walianzisha utafiti wa makampuni 100 bora yafanyayo biashara ya kiwango cha kati. Banki M Tanzania ndiye mdhamini mkuu wa tuzo zitakazotolewa baada ya utafiti huo muhimu. Utafiti huo hubainisha mafanikio ya makampuni yafanyayo biashara ya kiwango cha kati na jinsi yanavyochangia ukuaji wa uchumi kwa ujumla. Washindi wa utafiti huo watatangazwa katika hafla ya utoaji tuzo za makampuni bora yafanyayo biashara ya kiwango cha kati mwezi Septemba, hafla itakayofanyika jijini DSM.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa KPMG, Vincent Ongala alisema kuwa idadi ya makampuni ambayo yanajitokeza kwa hiari kushiriki katika utafiti huu inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. “tunatarajia kiasi cha makampuni 250 kushiriki katika tuzo za mwaka huu wa 2017.
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications, Bakari Machumu alielezea mafanikio waliyoyapata kutokana na kuandaa utafiti huu,” kuna makampuni ambayo hayatafanikiwa kushinda mwaka huu, lakini yasivunjike moyo kwani mwakani yanaweza kufanya vizuri zaidi.”Machumu pia aliwashukuru Bank M kwa kuendelea kuwaamini na kuendelea kuwa wadhamini wakuu kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Wadhamini wengine ambao wameshikana mikono na KPMG pamoja na MCL mwaka huu ni Azam Media.
AZAM MEDIA: Wamevutiwa kuungana mkono na wadhamini wengine ilikutoa fursa kwa wafanyabiashara 100 wa kiwango cha kati ilikuweza kupata fursa ya kutangaza biashara zao kupitia vyombo vyake vya habari ikiwemo Television na (Online as AZAM APP ONLINE). Hii ni fursa ya pekee kwa kutumia AZAM media unaweza kutanua wigo wa biashara katika nchi jirani kwani Azam Media imekuwa ikiangaliwa sana hapa nchini na nje ya nchi zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na baadhi ya sehemu kama nchi za kongo, Sudan. Hivyo itasaidia kupanua soko na kukuza biashara kwa bei nafuu ilikuwezesha kutangaza biashara kimataifa.