Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali na Wanajumuiya wa Chuo Cha Elimu ya Biashara wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Kikundi cha ngoma kutoka Jeshi la Polisi kikiongozwa na Afande Juma Boha Mnyaa kikitoa burudani ya ngoma ya asili ya ya Kibati kutoka Kusini Pemba wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es salaam.