
Mwenyekiti wa kamati ya mashinda ya Tunzo ya Ushairi nchini Tanzania Ibrahim Seushi akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tuzo hizo mapema hivi karibuni. Tuzo hizo zitaitwa Ebrahim Hussein ikiwa ni kumuenzi nguri na mkongwe huyo wa mashairi hapa nchini.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Hajaty Shani Kitoga akiimba shairi la Wakati Ukuta ambaole ni moja ya kazi za Profesa Ebrahim Hussein wakati wa uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizoanzishwa mapema hivi karibuni.