Uzinduzi Kipindi cha Mashariki Max

Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm akitoa hotuba ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Star Times katika nchi za Afrika Mashariki wakati wa hafla ya uzinduzi huo  jijini Dar es salaam.

Mtangazaji wa kipindi cha Mashariki Max kitakachorushwa kupitia Televisheni ya Star Times Jokate Mwegelo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Group nchini Langtang Lia

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Sekta ya michezo nchini inazidi kuimarika na kuongeza fursa kwa wanamichezo na wapenda michezo nchini kwa kuzileta pamoja nchi za Afrika ya Mashariki kwa kurusha ligi za michezo mbalimbali kutoka nchi hizo kupitia Televisheni ya Star Times.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Star Times Group kutoka Beijing China Michael Dearharm alipokuwa akitoa hotuba ya uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachorushwa kupitia televisheni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi kipindi hicho hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Bwa. Michael alisema kuwa Star Times Group wameamua kuanzisha kipindi hicho ambacho kinalengo la kuwaelimisha na kuburudisha wananchi wa nchi za Afrika ya Mashariki kwa kuwaunganisha kupitia michezo.
“Tumeamua na kudhamiria kuleta pamoja nchi za Afrika ya Mashariki kwa kuwaunganisha kupitia kipindi cha Mashariki Max na vipindi vingine vitakavyorushwa na TV yetu kwa mfumo wa digitali na kwa gharama nafuu kwa watumiaji wa huduma yetu” alisema Bwa. Michael.
Pamoja na kipindi cha Mashariki Max, vipindi vingine vitavyorushwa na TV hiyo ni ligi za mpira wa miguu kutoka nchi za Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi ambapo mpaka sasa kuna vituo vya kurushia matangazo vitatu katika nchi za Tanzania, Uganda na Kenya.
Zaidi ya ligi za nchi za Afrika Mashariki, kituo hicho cha TV kimejipanga kurusha matangazo ya ligi ya mpira wa miguu na michezo mingine kutoka nchi za Ujerumani, Italia na Ufaransa.
Kwa upande wake Mtayarishaji na Muandaaji wa vipindi mbalimbali vinavyorushwa na kituo hicho Roby Bresson alisema kuwa kituo chao kimejipanga kuendelea kuwaunganisha wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kurusha vipindi vyao kwa kutumia lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo kiunganishi kikuu katika mawasiliano miongoni mwa nchi hizo.
Aidha, Roby alisema kuwa nchi za Afrika zina mambo mengi mazuri ambayo dunia inapaswa kuyajua na kuyathamini badala ya dhana iliyojengeka kuwa bara la Afrika imegubikwa kwa mambo yenye mtazamo hasi tu.