Uwongo Wamfukuzisha Kazi Mkuu wa Mkoa Shinyanga…!

Anna Kilango Malecela

Anna Kilango Malecela

TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dk. John Pombe Magufuli amemfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa shinyanga Anna Kilango Malecela baada ya kutengua uteuzi wake kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa huo Ana kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.

Mkuu wa Mkoa huyu ni miongoni mwa wakuu wa mikoa ambao Rais Magufuli aliwateuwa hivi karibuni na kuwaasa wafanye kazi ipasavyo na kwamba hato sita kumchukulia hatua yeyote ambaye ataona kazi aliyopewa imemshinda. Mama Kilango anakuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kulamba machungu ya Rais Magufuli kutokana na msimamo wake wa kuzingatia umakini zaidi katika utendaji wake wa kazi.