Uturuki Kuisaidia Makumbusho ya Taifa Tanzania

 Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa chimbuko la Mwanadamu, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa chimbuko la Mwanadamu, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Balozi wa Uturuki nchini Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa Mila na Destuuri, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Balozi wa Uturuki nchini Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa Mila na Destuuri, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa Mila na Destuuri, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam. Nyuma kusho ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo Bw Achiles Bufure.

Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin ERALP akiwa kwenye ukumbi wa Mila na Destuuri, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam. Nyuma kusho ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo Bw Achiles Bufure.

Balozi ERALP (kushoto) akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula, katikati ni Mkuu wa Idara ya Program Bw. Chance Ezekiel.

Balozi ERALP (kushoto) akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula, katikati ni Mkuu wa Idara ya Program Bw. Chance Ezekiel.

Na Sixmund J. Begashe, Dar es Salaam
NCHI ya Uturuki imekubalia kuisaidia Makumbusho ya Taifa katika nyanja za Utafiti, Uhifadhi, Maonesho ya vioneshwa vya kimakumbusho na hata katika Maonesho mbalimbali ya muziki na sanaa ili kuboresha na kuendeleza shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Makumbusho ya Taifa nchini Tanzania.

Ahadi hii imetolewa na Balozi wa Uturuki hapa Nchini Mh Yasemin ERALP alipo kutana na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kubadilishana mawazo ili kuona ni kwa namna gani Ubalozi wake unaweza kushirikiana na Makumbusho ya Taifa.

Akiongea na Uwongozi huo wa juu wa Makumbusho nchini, Balozi ERALP alisema kuwa, Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu sana kwa utafiti, uhifadhi, uelimishaji na ustawi wa historia ya nchi yeyote ile husika, hivyo kwa Makumbusho ya Taifa la Tanzania haina budu kusaidiwa ili iweze kutimiza malengo hayo makuu kwa maslai ya watanzania na Dunia kwa ujuma.

Balozi ERALP aliongeza kuwa Ofisi yake, itaiunganisha makumbusho ya Taifa na Makumbusho mbali mbali za nchini Uturuki ili kutoa nafasi za wataalam wa Makumbusho zote kukutana na kubadilishana uzoefu wa kitaalam, na kuahidi kuleta wasanii kutoka Uturuki ili kufanya maonesho katika ukimbi wa kisasa wa maonesho uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Balozi huyo alipata nafasi ya kutembelea jengo la Makumbusho ya kwanzaTanzania la King George V lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam na kujionea namna jengo hilo linavyo hitaji ukarabati wa haraka, aliahidi kuwasiliana na Makampuni ya ujenzi ya Uturuki yaliyopo hapa nchini ili kusaidia ukarabati wa jengo hilo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho nchini, Prof. Audax Mabula amemshukuru balozi huyo kwa kuitembelea Makumbusho ya Taifa na kuonesha nia ya dhati ya kushirikiana na Makumbusho hiyo, pia ametoa wito kwa wadau mbali mbali wa ndani na nje ya nchi kushirikiana na Makumbusho ya Taifa ili kuboresha uhifadhi wa vyote vinavyo dhaminiwa na jamii ya hapa nchini.