UTSS Yatoa Changamoto kwa Redio za Jamii Juu ya Albino

Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa mwongozo kwa washiriki wa semina hiyo.

Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa mwongozo kwa washiriki wa semina hiyo.


DSC_0016

Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha mameneja wa Redio za jamii nchini (hawapo pichani) walioshiriki kwenye mafunzo ya siku moja ya kutoa elimu kwa Redio za jamii nchini juu ya kuandaa vipindi vyenye ujumbe sahihi wa masuala yanayohusu watu wenye Albinism iliofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema hivi karibuni. Katikati ni Afisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif na kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

OFISA mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS) Kondo Seif, ameitaka jamii kuungana kupiga vita imani potofu zinazosababisha mauaji kwa watu wenye albinism.

Alisema jamii ikiamka na kuamua kumaliza tatizo hilo, mauaji hayo yatakoma.

Kauli hiyo aliitoa katika semina ya siku moja ya elimu kwa Redio za jamii nchini juu ya kuandaa vipindi vyenye ujumbe sahihi ya masuala yanayohusu watu wenye Albinism iliofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani Mwanza hivi karibuni.

Kondo alisema katika jamii kumekuwa na imani potofu ambapo Albinism wamekuwa wakiitwa majina yanayolenga kunyanyapaliwa na kusababisha kushamiri kwa vitendo vya ukatili na mauaji dhidi yao.

Aliitaka jamii kutambua kuwa albinism ni hali ya ukosefu wa rangi asilia mwilini inayoathiri ngozi, macho na nywele na ni nadra hali hiyo kupatikana na haiambukizi kama watu wengine wanavyodhani.

Aidha ametaja jina sahihi la Kiswahili lililokubaliwa na baraza la Kiswahili Tanzania kuitwa watu wenye albinism kuwa ni watu wenye ualbino.

Alisema watu wenye ualbino wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kukosekana kwa taarifa sahihi zinawagusa wao kama ngozi kushindwa kuhimili jua, uoni hafifu na kupungua kwa usalama.

Kwa mujibu wa Takwimu za shirika hilo watu wenye Albinism zaidi ya albino 70 nchini Tanzania wameuawa, zaidi ya 30 wamekatwa viungo vyao na makaburi ya watu wenye Albinism 20 yamefukuliwa.

Ameviomba vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kutoa elimu sahihi kwa jamii ili kustawisha maisha ya watu wenye Albinisms kuwa kufanya hivyo maendeleo yao, jamii na taifa kwa ujumla yataimarika.

Awali akizungumza na washiriki wa semina hiyo Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliwataka waandishi wa habari kuzingatia matumizi sahihi ya lugha wanapoandika habari na kuandaa vipindi vinavyozungumzia masuala ya Albinism.

Pia amesisitiza kuandaa vipindi vinavyobeba ujumbe sahihi wa kuelimisha jamii juu ya masuala yanayohusu Albinism ili kubadilisha mitazamo ya jamii ili kuwathamini, kuwalinda, kuwaheshimu na kuwashirikisha katika maendeleo.

Sambamba na hilo amevitaka pia kubeba jukumu kubwa la kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura na kutoishia kujiandikisha tu bali wajitokeze kupiga kura kuwachagua viongozi ambao ni Madiwani, Wabunge na Raisi October 2015 pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa wakati ukifika.

Ameongeza katika matukio hayo muhimu ya kitaifa watu wenye Albinism wahamasishwe kushiriki kikamilifu vile vile na makundi mengine kama wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, wazee na makundi mengine maalum.

DSC_0031

Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akielezea dhima ya UNESCO kuwashirikisha shirika la Under The Same Sun (UTSS) kutoa elimu kwa Redio jamii ili kupaza sauti kwa jamii dhidi ya mauaji ya watu wenye Albinisim pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili walemavu wa ngozi.

DSC_0199

Afisa mtetezi na ushawishi kutoka shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun (UTSS), Kondo Seif akiendesha mafunzo kwa mameneja wa Redio jamii nchini (hawapo pichani) kwenye semina ya siku moja iliyofanyika wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza. Katikati ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

DSC_0055

DSC_0071

Meneja wa Redio jamii Mpanda FM iliyopo mkoani Katavi, Prosper Kwigize akichangia maoni yake kwenye semina hiyo namna ya kudhibiti mauaji ya watu wenye Albinism iliyofanyika hivi karibuni wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

DSC_0076

Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akielezea jitahada za kituo chake cha Redio kinavyoshiriki katika kukemea mauaji ya watu wenye Albinism kwa kuendesha midahalo mbalimbali pamoja na makala maalum kuhusiana na walemavu wa ngozi.

DSC_0013

Baadhi ya mameneja wa vituo vya Redio jamii nchini walioshiriki semina hiyo ya siku moja wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Bwana Kondo Seif (hayupo pichani) wa Shirika la Under The Same Sun (UTSS).

DSC_0008

DSC_0042

DSC_0233

Mkufunzi wa semina ya siku moja kwa Mameneja wa Redio jamii nchini Kondo Seif akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo. CHANZO modewjiblog