Uteuzi Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Masha J. Musomba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Uteuzi huo ulianza, Januari 22, 2015. Kabla ya uteuzi wake, Musomba alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).