Utafiti Waweka Bayana Changamoto za Wanawake Uchaguzi Mkuu

Pichani ni muonekano wa moja ya gazeti liloandika habari za unyanyasaji wa wanawake kipindi cha uchaguzi.

Pichani ni muonekano wa moja ya gazeti liloandika habari za unyanyasaji wa wanawake kipindi cha uchaguzi.

Na Mwandishi Wetu

UTAFITI mdogo uliofanywa katika baadhi ya vyombo vya habari ulibainisha kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Utafiti umeeleza kuwa kwa upande wa wanaume ni asilimia 88 ya vyanzo vya habari, huku katika habari zinazohusiana na uchaguzi, imeonekana wanawake bado waliendelea kubaki nyuma kwa asilimia 11 ikilinganishwa na asilimia 88 ya wanaume.

Akizungumza katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari na wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutoka makundi maalum iliyofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Hoteli ya GM Elegance, Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mark Gideon anasema kuwa wanaume waliongoza kutumika katika vyanzo vya habari katika magazeti yote yaliyofanyiwa tathmini ukilinganisha na wanawake.

Akifafanua tathmini yake kwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo, anasema kuwa vyanzo vingi vya wanawake vilifichwa. Anasema kuwa ilikua ni nadra sana kukuta habari za wanawake katika kurasa za mbele za magazeti na kusema kuwa magazeti mengi yalitoa habari nyingi za udhalilishaji na unyanyasaji wanawake wakati wa uchaguzi.

Baadhi ya washiriki katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari na wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutoka makundi maalum wakichangia mjadala.

Baadhi ya washiriki katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari na wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutoka makundi maalum wakichangia mjadala.

Aidha, anasema TAMWA inaimani kwamba ili kuondoa pengo la jinsia katika vyombo vya habari kuna haja ya kuongeza mafunzo ya usawa wa kijinsia, kibinadamu na haki za binadamu kwa ujumla kwa waandishi na yafanyike kabla ya uchaguzi ili waweze kuandika habari za uchaguzi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Anabainisha kuwa madawati ya uchaguzi katika vyombo vya habari yapatiwe mafunzo ya jinsia na kufanya Tathmini ya vyombo vya habari wakati wa uchaguzi ianze kufanyika mapema wakati wa chaguzi ndani ya vyama, wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi ili kuondoa tatizo la waandishi kurepoti habari za wanaume na kureport kwakiwango kidogo habari za wanawake.

Ofisa huyo wa TAMWA anaendelaaea kusema kuwa katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka jana vyombo vingi vya habari vilitumika kutoka na vyama vilivyokua kwani kulikuwa na vyombo vingine ambavyo hazitoi kabisa au kwa upendelea habari za upande mwingine wa chama kingine. Bw. Gideon anasema changamoto nyingine iliyojitokeza kipindi cha uchaguzi ni miundombinu mibovu kwa watu toka makundi maalum wakiwemo walemavu.

Baadhi ya washiriki katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari na wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutoka makundi maalum wakichangia mjadala.

Baadhi ya washiriki katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari na wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutoka makundi maalum wakichangia mjadala.

Anasema sehemu nyingine ilikosekana kabisa kitendo kilichochangia kundi hilo maalumu kushindwa kushiriki ipasavyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Anabainisha kuwa vyombo vya habari kutokufika maeneo ya pembezoni nalo lilikua ni tatizo ambalo lilifanya habari za wanawake wengi kuto fikiwa na waandishi. Kwa maendeo ya vijijini ilikuwa ni ngumu kwa wanahabari kuibua habari na ushiriki wao katika uchaguzi uliopita.

Ofisa Habari huyo wa TAMWA anaongeza kuwa kulikuwepo na changamato ambazo zilitokana na wanawake wenyewe kushindwa na kuto kuwa tayari kuhojiwa na vyombo vya habari pale walipotakiwa kufanya hivyo, na kuishauri taasisi hiyo kufanya mafunzo na mijadala endelevu na sio kungojea kipindi cha uchaguzi ili kuwajengea uwezo wanawake waeze kuzungumza pale wanapotkiwa kufanya hivyo.

Ofisa Habari wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mark Gideon (kulia) akitoa tathmini katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari na wagombea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, kutoka makundi maalum.

Hata hivyo anatoa wito pia kuwepo kwa waandishi maalum wa kuripoti habari za uchaguzi na masuala ya siasa ili kuwajenga zaidi wataalamu wa kuandika na kuchambua habari hizo wakati wa uchaguzi. Hili litasaidia vyombo vya habari kuvichimba vizuri vyama na wagombea wake wakati wa uchaguzi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana (2015) Tamwa kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN WOMEN ilikua ikitoa mafunzo ya kujengea uwezo makundi maalum wakiwemo wanawake, walemavuna, vijana ili waweze kushiriki ipasavyo kwenye uchaguzi huo.