Timu kubwa za Ujerumani vitashuka dimbani huku wenyeji Borussia Dortmund wakilenga kuongeza moto katika kinyang’anyiro cha taji la Bundesliga kwa kupunguza hata zaidi pengo kati yao na Bayern Munich
Vijana wa Pep Guardiola walionekana ni kama wananyakua kombe lao la nne mfululizo, wakati wakiwa na pengo la pointi nane dhidi ya Dortmund, hadi pale Mainz walipowawekea breki kwa kuwachapa mabao mawili kwa moja Jumatano usiku.
Dortmund nayo iliishinda Darmstadt 2-0 na sasa kivumbi cha leo uwanjani Signal Iduna Park kinatarajiwa kuwa cha kusisimua isipokuwa Bayern wanapigiwa upatu. Wakati timu hizo zilikutana mara ya mwisho Oktoba, Bayern iliizaba Dortmund 5-1 mjini Munich.
Kando na kinyang’anyiro cha kutaka ubingwa, kutakuwa pia cha kuepuka kushushwa ngazi wakati Werder Bremen watawaalika washika mkia Hanover. Hoffenheim ambao watasafiri kupambana na Stuttgart.
Katika mechi nyingine za leo, Wolfsburg watapambana na nambari nne Borussia Moenchengladbach, VfB Augsburg watapiga dhidi ya Bayer Leverkusen, Eintracht Frankfurt dhidi ya Ingolstadt, Cologne watakuwa nyumbani dhidi ya Schalke.
Kesho Jumapili, Mainz watapambana na Mainz v Darmstadt, wakati Hamburg wakipambana na nambari tatu kwenye ligi Hertha Berlin