Usalama Barabarani Wamtangaza Athuman Hamis Kuwa Balozi Wao

IMG_0093
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira A. Silima (kushoto) akizungumza na wanahabari pembeni yake ni Athuman Hamis balozi wa Usalama Barabarani.

IMG_0095
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira A. Silima (katikati) akizungumza na wanahabari, Kushoto ni Kamanda wa Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga, wakiwa na Athuman Hamis, Balozi wa Usalama Barabarani (kulia).

IMG_0097

 

Kutoka kushoto ni Kamanda wa Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira A. Silima na Athuman Hamis ambaye ni Balozi wa Usalama Barabarani (kulia).

Na Joachim Mushi

SERIKALI kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi (Trafiki Polisi) Tanzania imemtangaza mwanahabari Athuman Hamis kuwa balozi atakayekuwa na kazi ya kutangaza madhara ya ajali barabarani kwa umma nchini Tanzania.

Hamis ambaye ni miongoni mwa Watanzania kadhaa waathiriwa wa ajali za barabarani nchini Tanzania aliwahi kupata ajali ya gari akiwa kazini safarini ambayo ilimsababishia kuwa mlemavu asiyejiweza kuendesha shughuli zake kama ilivyokuwa hapo awali.

Akimtangaza mwanahabari huyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira A. Silima alisema wameamua kuwatumia mabalozi kusambaza jumbe za usalama barabarani ili kuonesha uhalisia na namna ajali inaweza kubadili maisha ya mtu na hata kuwa tegemezi maishani.

Alisema watu kutofuata sheria za barabarani kuna madhara makubwa kwa watu wenyewe na taifa kupoteza mali na nguvu kazi hivyo Serikali kutumia mbinu mbalimbali kama ilivyo sasa kuhakikisha inamaliza ajali za barabarani.

“…Tumeamua kutumia mbinu hii ya mabalozi kwani tumeona uenda ikawa na manufaa ya kufikisha ujumbe zaidi, tumekuwa tukiona inatumia maeneo tofauti na kuwa na mafanikio,” alisema Naibu Waziri Silima akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Kwa heshima hiyo sasa Hamis atakuwa akitumika kutoa jumbe mbalimbali za kuzingatia usalama barabarani ili umma uelewe namna gani ajali inaweza kumwasiri mtu mwenye viungo kamili na kuwa tegemezi baada ya ulemavu wa ajali tofauti na alivyokuwa hapo nyuma.