Dirisha la Usajili la Wachezaji Linavyotikisa Ulimwengu wa Soka

pogba

Klabu ya Manchester United inam’mezea mate Paul Pogba lakini hakuna mpango wowote wa kuonyesha kuna mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo yameanza.

Uvumi umekuwepo kuhusu uhamisho wa mchezaji huo wa pauni milioni 100 unaotarajiwa kuvunja rekodi ya dunia,lakini imebainika kuwa hakuna mazungumzo yoyote yalioanza kati ya Manchester United na Juventus

Ahmed Musa

Klabu ya Leicester City imemsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa kandarasi ya miaka 4 itakayogharimu pauni milioni 16.

Southampton,Everton na West Ham walikuwa wakitafuta saini ya mchezaji huyo.
Musa ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Leicester baada ya kipa Ron-Robert Zieler ,beki Luis Hernandez na kiungo wa kati Nampalys Mendy.

Mchezaji huyo alijiunga na CSKA mwaka 2012 na kufunga mabao 54 kati ya mechi 168 alizocheza,na amefunga mabao 11 katika mechi 58 alizochezea Nigeria tangu aanze kucheza mwaka 2010.

PetrCech2

Mlinda lango wa Arsenal Petr Cech ambaye ni raia wa Jamhuri ya Czech ametangaza kuwa amestaafu katika soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ndiye mchezaji aliyelichezea sana taifa lake kupitia mechi 121 alizoshirikia tangu aanze mwaka 2002.

Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Czech ambacho kilifika nusu fainali ya Euro2004 kabla ya kushindwa na mabingwa Ugiriki.

_78365113_pep_guardiola_getty3

Mkufunzi mpya wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa alienda nchini Uingereza kuthibitisha kuwa inawezekana kucheza mchezo mzuri katika ligi ya Uingereza.

Gurdiola mwenye umri wa miaka 45 ambaye ametia kandarasi ya miaka mitatu ,amesema kuwa alipendelea kusalia kuifunza Bayern Munich ,lakini alitaka mtihani mwengine katika ukufunzi wake.

Raia huyo wa Uhispania amekiri kwamba alikuwa na kila alichohitaji wakati alipokuwa Barcelona ,lakini akakana kuwa huenda anakabiliwa na kibarua kigumu katika klabu ya Manchester City.

_87945478_jurgen_klopp_liverpol_reuters

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ameweka kandarasi mpya ya miaka sita na mmiliki wa klabu hiyo akisema ingekuwa makosa kutompatia kandarasi ndefu.

Klopp alijiunga na Liverpool mnamo mwezi Oktoba ,baada ya kukubali mkataba wa pauni milioni 15 ambao umeongezwa hadi mwaka 2022