Usajili uliokamilika hadi dakika Hii, na Zilizogonga Mwamba Soma Hapa

Chicharito

Gazeti la The Times limewashtua watu kwa kuandika taarifa zinazo ihusisha Liverpool na mchezaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez ‘Chicharito’.

Ripoti zinasema kwamba, Liverpool imejadili kusajili mshambuliaji mwezi huu, lakini wekundu hao wanaamini kwamba Bayer Leverkusen hawatakuwa tayari kumwachia nyota huyo.
The Times think Chicharito will command a fee of £20 million. The Times inadhani Chicharito atahitaji £20 millioni kama ada ya uhamisho
Hata kama dili hilo lisipofanikiwa, lakini ukweli utabaki palepele kwamba Liverpoo bado inahitaji mshambuliaji

ram

kiungo wa kati wa Chelsea Ramires amehamia klabu ya Uchina Jiangsu Suning. Ripoti zinasema Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 28 amenunuliwa £25m.

Alitia saini mkataba mpya wa miaka minne Chelsea Oktoba mwaka uliopita lakini alianza mechi saba pekee za Ligi kuu ya uingereza msimu huu akiwa na Klabu ya Chelsea.

Jiangsu walimaliza nafasi ya tisa katika ligi kuu ya Uchina 2015 na mkufunzi wao ni Beki wa zamani wa Chelsea Dan Petrescu.

Ramires alisaidia Blues kushinda Ligi kuu, Kombe la FA, Kombe la Ligi, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Uropa Ligi,Kwa jumla, alichezea Chelsea mechi 251, na kuwafungia mabao 34 kipindi alichokaa Stamford Bridge. Ramires alinunuliwa £17m na Chelsea kutoka Benfica mwaka 2010.

sand

Nao Klabu ya soka Newcastle United imesajili winga wa kimataifa wa Uingereza Andros Townsend kwa gharama ya pauni milioni 12 akitokea Tottenham Hotspur.

Winga huyu mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano kukitumikia kikosi cha Newcastle chini ya meneja Steve Mclaren.

Townsend amecheza michezo mitatu ya msimu huu akitokea benchi huku akiondolewa katika kikosi kilichokua kinashiriki michuano ya Europa ligi baada ya kugombana na kocha wa viungo Nathan Gardiner.

Meneja wa Newcastle United Steve McClaren, Amesema”kumleta winga huyu katika timu hiyo ni usajili mzuri na mkubwa, Andros ni aina ya mawinga wanaocheza staili ya kizamani anaweza cheza kulia na kushoto .”

Townsend alijiunga na kituo cha michezo cha Spurs akiwa na miaka nane na alianza kukitumiki kikosi cha kwanza katika msimu wa 2013-14.

ahmed_musa

Kwa upande wa Leicester bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa licha ya ombi lao la hapo awali kukataliwa na kilabu ya CSKA Moscow.

Kilabu hiyo ya Urusi imekataa ombi la dola milioni 21.6 huku wakitaka kiasi cha dola milioni 27 kumuachilia mshambuliaji huyo.Mchezaji huyo yuko tayari kujiunga na kilabu hiyo.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Nigeria ana thamani ya dola milioni 32 katika kandarasi yake ambayo inakamilika mwaka 2019.
Leicester inatarajiwa kurudi kwa CSKA na kiasi cha juu ili kumchukua mchezaji huyo kabla ya kipindi cha dirisha la uhamisho kukamilika tarehe 1 mwezi Februari.

malouda

Kilabu ya Misri Wadi Degla imemsajili aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na Chelsea Florent Malouda.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 amejiunga kutoka kilabu ya Delhi Dynamos nchini India ambapo amekuwa akisakata soka yake tangu mwaka 2015 mwezi Agosti.

Ameandikisha mkataba hadi mwisho wa msimu na anajiunga na mchezaji mwenzake wa Ufaransa Patrice Carteron ambaye alikuwa mkufunzi wa kilabu hiyo mapema mwezi Januari.

Malouda ambaye ameichezea Chelsea kutoka mwaka 2007 hadi 2013,aliichezea Ufaransa mara 80 na kufunga mbao tisa ya kimataifa.

mbia

Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina.
Mbia amekuwa akichezea Trabzonspor ya Uturuki.

Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 29 sasa atajiunga na nyota wa Ivory Coast Gervinho katika klabu hiyo ya Uchina. Gervinho alijiunga na Hebei China Fortune akitokea AS Roma Jumatano.
Twamsubiri sana beki kamili Mbia afike hapa na kuonyesha ustadi wake,” klabu hiyo iliandika kwenye Twitter.
Mbia aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Najivunia kujiunga na Hebei China Fortune, niko tayari. Twende kazi.

samata

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ametambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Genk ya Ubelgiji.

Samatta amejiunga na klabu hiyo inayocheza Ligi Kuu ya Ubelgiji kutoka kwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Samatta, aliyetawazwa mchezaji bora wa mwaka Afrika 2015 kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, ametia saini mkataba wa hadi mwisho wa msimu wa 2019/2020.

pato

Chelsea imemchukua mshambuliaji wa Brazil Alexandre Pato kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 26 ambaye amekuwa akichezea klabu ya Corinthians ya Ugiriki amechezea taifa lake mechi 27 na kuwafungia mabao 10.

Alichezea Brazil katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008 na 2012. The Blues, walioshinda Ligi ya Premia msimu uliopita, wametatizika sana msimu huu na wamo nambari 13 ligini, ingawa bado wanacheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kaimu meneja Guus Hiddink amesema licha ya hali kwamba Pato ametatizwa sana na majeraha, hadhani kwamba kumchukua ni kucheza bahati nasibu.

adebayo

Mshambuliaji wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor akiwa ameshika jezi ya Crystal Palace baada ya kukamilisha uhamisho wake kwa Mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu, ambao unaweza kuongezwa iwapo atafanya vizuri. Adebayor amekuwa nje ya Uwanja tangu mwanzoni mwa msimu baada ya kuachwa Tottenham Hotspur ingawa itaendelea kumlipa Pauni 30,000 kwa wiki badala ya 100,000 kwa sababu bado ana Mkataba nayo.