Upinzani Liberia kuyakataa matokeo ya uchaguzi

Vyama ninane vya upinzani, vikiwemo viwili ambavyo ni wapinzani wakuu wa Rais Ellen Johnson-Sirleaf vimesema kuwa vitayakataa matokeo ya uchaguzi wa urais uliyofanyika wiki hii vikidai kuwepo kwa wizi mkubwa wa kura.
Kwa mujibu wa matokoe yaliyotolewa Ijumaa iliyopita, Rais Johnson-Sirleaf anaongoza kwa 45.4 ya kura dhidi ya mpizani wake mkuu Winston Tubman wa chama cha CDC aliyepata 29.5 asilimia ya kura.Hata hivyo Rais Johnson-Sirleaf hana wingi wa kura zinazohitajika ili kuweza kushinda moja kwa moja uchaguzi huo.
Tume ya uchaguzi ilisema kuwa karibu nusu ya kura zote zimekwishahesabiwa.Uchaguzi huo uliyofanyika Jumanne wiki hii ulikuwa wa amani ambapo mpaka sasa hakuna waangalizi wowote waliyoelezea kasoro zozote kubwa zilizojitokeza katika mchakato mzima.

-DW