Unyama: Mwenyekiti wa Kijiji Auwawa, Viungo Vyake Vyapikwa

Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti wa cha Songambele wilayani Mlele mkoani Katavi wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti wa cha Songambele wilayani Mlele mkoani Katavi wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.

NI unyama wa kutisha umetokea katika Kijiji cha Songambele wilayani Mlele mkoani Katavi watu wawili wamemvamia Mwenyekiti wa Kijiji cha Songambele kisha kumuuwa kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili na sehemu zake za siri.

Watu hao pia walimkata mkono wake mara mbili baada ya kufanya unyama huo kabla ya kuchukua viungo walivyokata kata kisha kuvitia kwenye sufuria, kuweka maji na kubandika kwenye moto na kuanza kuvipika.

Baada ya Tukio hilo watu hao walitokomea sehemu isiyofahamika, lakini taarifa ambazo zimepatikana baadaye jana jioni tayari polisi wilayani Mlele wamewakamata watu hao wakijaribu kuvuka kukimbilia mkoani Tabora. Watuhumiwa wanadaiwa kutenda tukio hilo majira ya saa saba za usiku. Samahani hatukuweza kutumia picha hizo kwasababu ya maadili.

Wakati huo huo; taarifa iliotufikia zinasema kwamba askari polisi namba G.6352, Abduel wa wilayani Ludewa akiwa lindo Benki ya NMB alipigiwa simu na mpangaji mwenziwe kuwa chumba chake kimevunjwa na kuibiwa ndipo alipo toka lindoni kuelekea eneo la tukio lakini akiwa njiani alikutana na watu wakamwambia moja ya vitu vyake vilivyoibwa (TV) imeibiwa na January Boni.

Askari huyo akiwa na watoa taarifa waliongozana hadi Boni na kumwambia amrejeshee TV yake lakini muhusika aliingia ndani na kutoka na panga na kutaka kumkata askari ndipo askari akakoki silaha yake na kumpiga muhusika risasi ya kifuani na kutokezea mgongoni na kupoteza maisha papo hapo. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.