UNIDO Yaahidi Kuongeza Ushirikiano na Tanzania

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) nchini Tanzania, Emmanuel Kalenzi akifafanua shughuli za Shirika hilo na mafanikio yake hapa nchini ambapo mpaka sasa limeshachagua maeneo yatakayofadhiliwa chini ya ‘Global Environment Facility- GRF’ kwa miradi kadhaa katika mikoa ya Morogoro, Njombe na Rukwa.
Akizungumza wakati wa wiki ya maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa amesema katika kutimiza malengo ya UNIDO ambayo ni kukuza uzalishaji viwandani na kupunguza umasikini, shirika hilo linafanya kazi bega kwa bega na serikali na jamii kwa ujumla katika kuongeza ushiriki wa wananchi katika vikundi ili kurahisisha maendeleo.