Ofisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya Wilayani Karagwe Mwalim Emmanuel Muganyizi kuhusiana na umuhimu wa wanfunzi wa shule yake kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa na faida zake.
Ofisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ndama na kuwapa hamasa ya kuwa walezi wazuri wa vilabu hivyo vitavyoanzishwa shuleni hapo ikiwa ni kama somo la ziada kwa wanafunzi wao ili wasipate muda wa kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
Usia Nkhoma Ledama akiongozwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya wilayani Karagwe kuelekea madarasani kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Ofisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama aliwaelezea wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndama, wilayani Karagwe mkoani Kagera, umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa (UN Club) vinavyoanzishwa mashuleni kwa kuwa kwanza vitawasaidia kujitambua.
Amewaambia kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu hivyo mashuleni kujiunga kwa wingi zaidi na kutawawezesha kujifunza shughuli za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.
Bi. Usia pia amewafafanulia vijana kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya kazi za kujitolea.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndama wakimsikiliza kwa makini Ofisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
Usia Nkhoma Ledama katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndama pamoja na Mkurugenzi wa Radio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe Bw, Joseph Sekiku (kushoto).
Ofisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akijitambulisha kwa baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Kushoto mwenye suti ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Johnbosco Paul.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akikagua Maktaba ya Shule ya Sekondari Kayanga. Kulia ni Mwl. Mkuu wa Shule ya Kayanga Johnbosco Paul.
Ofisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya sekondari ya Kayanga amewaelezea kuwa pindi watoto wao wanapojiunga na klabu za Umoja wa mataifa zilizopo mashuleni watapata elimu na uzoefu utakaotengeza thamani ya CV zao na kuzipa uzito zaidi na pia watapata ufahamu wa mambo mengi utakao wasaidia wasijiunge na vikundi visivyofaa wala kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
Amewaambia wazazi hao ndani ya klabu hizo hutokea kupata tarajali, uzoefu wa kazi, na kwamba kwa kupitia klabu hizo vijana wote shule zilizopo mikoa yote ya Tanzania watakuwa na nafasi ya kuwa karibu na taratibu na kanuni za Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakiwa mapumzikoni kuelekea kupata uji.