SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.
Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.
Misaada hiyo kwa pamoja ilikabidhiwa Jumamosi iliyopita katika halfa ambaye mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
Majaliwa alishuruku UNFPA kwa msaada huo na kutaka utumike vizuri ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
“ Nimeona vifaa vya hospitali vingi na vya gharama kubwa, sasa ni wajibu wetu kuvitunza na kuvitumia vizuri. Mfano gari tu limegharimu shilingi milioni 80. Huu ni msaada mkubwa sana na kwa niaba ya serikali nawashukuru sana UNPFA, tutaendelea kushirikiana”, alisema Majaliwa .
Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwaagiza vingozi wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbogwe kuhakikisha kuwa gari hilo linatumika kusafirisha wagonjwa tu na sio vinginevyo.
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.
“ Gari hili litumike kwa matumizi ya wagonjwa tu. Sitegemei kusikia kuwa linapeleka wafanyakazi sokoni kununua nyanya. Na Mkurugenzi atenge bajeti ya mafuta ya gari hili muda wote”, aliagiza Majaliwa.
Hafla ya makabidhiano ya misaada hiyo ilienda sambamba na maadhimisho ya siku ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa Fistula duniani yaliyofanyakia kitaifa katika viwanja vya shule ya msingi Masumbwe katika Wilaya ya Mbogwe , Mkoani Geita.
Akizungumuza katika hafla hiyo Mwakilishi msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dkt. Rutosha Dadi alisema msaada wa vifaa walivyotoa utasadia kumaliza tatizo la Fistula na kuboresha huduma zingine za afya .
“ Tumefanya ukarabati mkubwa sana katika jengo la upasuaji na kutoa vifaa vya kisasa kama vile Ultrasound”, alisema Dkt. Dadi.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha (wa nne kulia) akitoa salamu na kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na umati wa wakazi wa Mbogwe waliokusanyika kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa miradi ya AMREF, kanda ya ziwa Dkt. Awene Gavyole, Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, Katibu Tawala wa mkoa wa Geita, Charles Palanjo, mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa, Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita, Joseph Kisalla, Grace Lyon pamoja na Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Mbogwe mkoa wa Geita.
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akisisitiza jambo wakati wa kutoa salamu za Umoja wa Mataifa.
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla akizungumza na wakazi wa Mbogwe ambapo aliwataka kufika katika vituo vya afya vilivyokaribu na makazi yao kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Fistula pindi wanaonapo dalili na moja kwa moja kuwasiliana na Hospitali yake inayotoa huduma za matibabu bure ikiwemo usafiri na malazi mpaka mgonjwa anapopona na kumrejesha anakoishi.
Bi. Esther Ernest akitoa ushuhuda wake baada ya kuteseka na ugonjwa wa Fistula kwa takribani miaka 8 na jinsi jamii ilivyomnyanyapaa akiwemo mume wake hadi alipopatiwa matibabu na kupona kabisa hali iliyompelekea kurudisha furaha na nuru katika uso wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Kikundi cha maigizo cha Mrisho Mpoto kikitoa elimu kwa njia ya maigizo jinsi Wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula wanavyonyanyapaliwa na waume zao na kudhalilishwa kwa jamii ikiwemo kuitwa majina ya kila aina kutoka na kutokwa na haja ndogo muda wote bila breki.
Mwigizaji wa kikundi cha sanaa za maigizo cha Mrisho Mpoto akilia kwa uchungu kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula na kunyanyapaliwa na mumewe wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Msanii mahiri wa sanaa ya kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akimliwaza Mwanamke anayenyanyapaliwa na mumewe kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula ambao unatibika bure kabisa bila gharama yoyote na Hospitali ya CCBRT.
Mume wa mwanamke anayeumwa Fistula wakisoma vipeperushi vya CCBRT vinavyotoa elimu, dalili na nini cha kufanya pindi unapojigundua ni Fistula pamoja na jirani yake wakati wa mchezo wa maigizo kwenye maadhimisho hayo.
Mrisho Mpoto akiendelea kutumia sanaa ya maigizo kuelemisha umati wa wakazi wa wilaya ya Mbogwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifurahi jambo kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza Balozi wa Fistula CCBRT, Elizabeth Jacob na kumkabidhi pesa taslimu Sh. 20,000/- kama motisha ya kazi anazofanya za kuwasafirisha wagonjwa wa Fistula jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Balozi wa Fistula CCRT, Elizabeth Jacob akionyesha pesa alizokabidhiwa kama zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Kassim Majaliwa.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza na kumkabidhi pesa taslimu sh. 100,000/ kama motisha ya kazi anazofanya za kuelimisha jamii kwa kutumia sanaa na maigizo Mrisho Mpoto aliyekuwa akisheresha sherehe hizo.
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla ( kushoto) na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kulia) wakimuangalia mtoto Nyambole Kulubone mwenye tatizo la mdomo wa Sungura akiwa amebebwa na mama yake Mariam Sanda (22) Mzazi huyo aliyehudhuria katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula aliahidiwa na Bi. Haika Mawalla (kushoto) mtoto wake atatibiwa bure katika hospitali CCBRT baada ya kusikia matangazo jirani na eneo liliofanyika sherehe hizo ambapo kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita.
Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbongwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
Burudani kutoka kwenye kikundi cha Mrisho Mpoto.
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Petr Shilogile (kushoto) akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa uliofadhiliwa na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania na ujenzi kusimamiwa na AMREF kabla ya kuzinduliwa rasmi. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuzindua cha jiwe la msingi huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi (kulia) akishuhudia tukio hilo.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua jengo la upasuaji huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akishuhudia tukio hilo.
Sasa limezinduliwa rasmi.
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile (kulia) akitoa maelezo kwenye chumba cha kujifungulia kina mama kilichowekwa vifaa vyote muhimu kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
Wafadhali wa ujenzi na vifaa kwenye kituo hicho Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa baada ya kuzinduliwa kituo hicho cha afya. Kulia ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile.
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akielezea changamoto waliozokuwa nazo hapo awali za kipimo cha “Ultra sound” kilichonunuliwa na UNFPA ambacho hivi sasa kitapatikana kituoni hapo kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
Mh. Kassim Majaliwa na Dkt. Rutasha Dadi wakipiga makofi.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akijaribu gari hilo.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akitoa angalizo la matumizi mabovu kwa DED wa Mbogwe na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi funguo za gari hilo la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, Abdala Idd Mfaume.
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mara baada ya makabidhiano hayo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Muhanga wa Fistula, Bi. Ester Ernest (walioketi kulia), Balozi wa Fistula CCBRT, Bi. Elizabeth Jacob (wa pili kushoto), Katibu Tawala mkoa wa Geita, Charles Palanjo (kushoto) na waliosimama kutoka kushoto ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, MC.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)