Na Mwandishi Mwetu
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), limewaomba wadau wa habari hasa wa matumizi ya intaneti kuzingatia maadili na usiri katika kazi zao ili kutovunja sheria zilizowekwa na mamlaka husika likiwemo suala la sheria ya mtandao iliyopitishwa hivi karibuni nchini Tanzania.
Hayo yameelezwa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliyekuwa akimwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues katika Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao (NIGF), lililofanyika mwishoni mwa wiki na kuandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
UNESCO inaamini masuala ya usiri katika mitandao ni njia bora zaidi za kuepukana na suala la mmomonyoko wa maadili na usio zingatia taaluma.
Ambapo amebainisha kuwa, takribani Asilimia 84 ya Mataifa duniani wamegundua hawana sheria madhubuti ya kulinda uhuru wa usiri kwa wananchi kupitia mitandao hivyo ni muhimu kuzingatia taaluma na maadili kwenye matumizi ya intaneti hasa kwa kipindi hichi.
“UNESCO inaamini mambo muhimu ya kuzingatia juu ya matumizi ya mitandao ikiwemo kuwa na Uwazi, Upatikanaji na Ushirikishi. Kwa hayo machache, mjadala huu wa matumizi ya mtandao unaweza kufanikiwa na sie tunapenda kuungana na nyinyi katika kushirikiana katika suala hili” alieleza Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday Richard akifungua rasmi Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao (NIGF) lililoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano COSTECH jijini Dar. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO na kulia Mwenyekiti wa National Governance Internet Forum, Kenneth Simbaya.
Aidha, katika mkutano huo, imeelezwa kuwa, matumizi makubwa ya mtandao wa kompyuta (intaneti) yatasaidia ongezeko la pato la taifa (GDP).
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya jukwaa la mtandao wa intaneti (IGF) Kenneth Simbaya wakati wa jukwaa hilo ambapo amebainisha kuwa, katika matumizi yake ni muhimu sana kujadili kutengeneza kesho wanayoitaka watanzania katika matumizi ya mtandao.
Ameeleza chombo cha IGF kimelenga kuangalia maendeleo ya mtandao nchini usalama wake na matumizi ya mtandao yanayoelenga kubadilisha maisha ya watanzania kwani chombo hicho nchini Tanzania kimeundwa kutokana na mkutano wa kimataifa wa jamii ya wanahabari (WSIS) waliotaka kuwepo na jukwaa kuangalia matumizi ya matandao kutokana na kuongeza kwa haja ya matumizi.
Simbaya amesema Majukwaa hayo yanatakiwa kuzungumza kuhusu sera kwa lengo la kuangalia uendelevu wake , usalama, ukuaji wa mtandao wenyewe na menejimenti yake.
Kwa upande wake Mtaalamu kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh akithibitisha umuhimu wa mtandao katika maisha ya sasa na yajayo, alielza kwamba kama kutakuwepo na ongezeko la watumiaji angalau kwa asilimia 10 pato la taifa litaongezeka kwa asilimia 1.4. zaidi.
Ambapo anaendelea kubainisha kuwa, kwa sasa idadi ya watumiaji wa mtandao wameongezeka kufikia asilimia 11 na kwamba lugha ya mtandao kwa sasa inaathiri watu mbalimbali kwa namna njema na namna mbaya.
Jukwaa hilo pamoja na kuzungumza kuhusu uendelevu wake pia ulizungumzia sheria , kanuni na taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa katika matumizi na utawala wa intaneti ili kuzifanya zitumike kwa makusudio mema zaidi.
Naye mtaalamu wa masuala ya mtandao wa intaneti, Maxence Melo kutoka Jamii Forum amesema kwamba mpaka sasa anaona kwamba matumizi ya mtandao Tanzania bado salama ingawa juhudi lazima ziendelee kufanyika kuhakikisha kwamba hali ya usalama inaendelea kuwapo.
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO akitoa salamu za shirika la UNESCO wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao (NIGF) ulioandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Katibu Mtendaji wa Tanzania Education and Research Network (TERNET), Amos Nungu akitoa salamu za TERNET kwa wadau waliohudhuria jukwaa hilo.
Mtaalamu kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh akiwasilisha mada iliyoelezea umuhimu wa mtandao katika maisha ya sasa na yajayo wakati wa jukwaa hilo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki waliohudhuria jukwaa hilo wakifuatilia “presentation” iliyokuwa ikitolewa na Mtaalamu kutoka TCRA Dk. Emmanuel Manasseh (hayupo pichani).
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph kwa mtaalamu kutoka TCRA (hayupo pichani) kama wana mipango gani kuhakikisha kuwa kutakuwepo na masafa ya kutosha kwa miaka mingi ijayo kwaajili ya wananchi wa vijijini na wale wasio na uwezo.
Picha ya pamoja.
Maxence Melo kutoka Jamii Forum akizungumza na waandishi wa habari wakati wa jukwaa lililowakutanisha kwa pamoja wadau wa masuala ya mitandao ya intaneti.
Maxence Melo kutoka Jamii Forum (katikati) akipata picha ya pamoja na wajumbe wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Fredy Njeje wa Blog za Mikoa (kulia) na Mr. Verbs.