Na Ferdinand Shayo
Watu wengi hutumia muda wao baada ya kazi kukaa na marafiki,makundi rika na wengine hufanya mambo ambayo huwazuia kuzifikia ndoto zao.
Wengine hutumia muda wao baada ya kazi kuongeza vipato vyao kwa kufanya miradi binafsi ,kuongeza maarifa kwa kujisomea vitabu na majarida mbalimbali ,kuhudhuria semina,mafunzo na makongamano.
Muda unaoutumia baada ya kazi unaweza kukuongezea mafanikio au kukupunguzia mafanikio yako katika maisha.
Muda unaotumia baada ya kazi unaweza kukuongezea maisha au kukupunguzia maisha kulingana na yale unayoyafanya.
Simaanishi uwe bize masaa 24 hapa naongelea yale masaa kadhaa baada ya kazi ambayo watu huyatumia kujiachia ,kujistarehesha,kujipumzisha baada ya kazi jambo ambalo ni zuri si vibaya .
Muda huo watu wengine huutumia kufanya maongezi ambayo ni hasi huyaharibu mafanikio yao na kuwazuia kuingia kwenye mafanikio yao.
Baada ya kazi kuna vitu vingi unaweza kuvifanya ambavyo unavipenda kama vile kujifunza ala za muziki,kujisomea kuongeza maarifa maana bila maarifa watu huangamia hata kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa “watu wangu huangamia kwa kukosa maarifa”.
Tunapaswa kujijengea tabia ya kutafuta maarifa kwa kujisomea ,kusikiliza ,video,sauti ambazo zinakupa maarifa ya kujenga familia,jamii na taifa.
Watu wengi hukosa muda wa kujitafuta wewe ni nani?,kwanini uko duniani?,unapaswa kufanya nini? Pia kujitafakari na kujitathmini wamezidiwa na mbio za maisha ,kazi na marafiki hivyo kujikuta akikimbizana na kazi na kuacha kukimbiza ndoto zake.
Kuwa na mwendo wa kasi katika maisha ni kitu muhimu lakini kwenda kasi bila kuwa na mwelekeo si kitu,weka dira yako ama mwelekeo wako kadiria mbio zako kisha kimbilia ndoto zako mpaka uzifikie.
Wengine hujikuta wakitafuta furaha maishani mwao na kujikuta wakikimbizana na furaha kwa kudhani kuwa wakipata kitu Fulani watakua na furaha wanakipata hicho lakini bado hawapati utoshelevu ndani yao.Wanatafuta vitu vingi wanavipata au kuvikosa lakini hawapati furaha ya kutosheleza .
Hatujui ya kuwa furaha haitokani na wingi au uchache wa vitu ulivyonavyo,furaha ya kweli ni kuwa na amani ya kweli na kuridhika na vile ulivyonavyo haijalishi na vingi au vichache.
Watu wengi hufanya kazi masaa machache huku wakitumia masaa mengi kujipumzisha ,kupiga zogo,kujistarehesha ,kutembea na marafiki,makundi yasiyofaa ndio maana mafanikio kwao yanabaki kuwa ndoto.
Ndege wanaofanana huruka pamoja,Nakutakia mafanikio katika maisha yako
ferdinandshayo@gmail.com
0765938008