MWANDISHI wa BBC Bashir Sa’ad Abdullahi ambaye yupo katika eneo la mlipuko amesema ghorofa ya chini ya jengo hilo imeharibika sana. Huduma za dharura zinaondoa miili ya watu kutoka katika jengo hilo huku majeruhi wengine wakipelekwa hospitali, anasema mwandishi wetu.
Makundi ya wanamgambo wa Kiislam wamekuwa wakifanya mashambulio katika jiji hilo katika siku za hivi karibuni. Bomu la kutegwa ndani ya gari lililipuka katika kituo cha polisi mwezi Juni na kulaimiwa kundi la Boko Haram, kundi ambalo linataka Nigeria kuanzisha matumizi ya sheria za Kiislam, Sharia.
Hakuna kundi lililokiri kufanya shambulio la siku ya Ijumaa, lakini maofisa wa Serikali wamelaumu “magaidi” kwa shambulio hilo, anasema mwandishi wetu. Watu walioshuhudia wamesema bomu la kutegwa ndani ya gari lililipuka, lakini taafifa nyingine zaidi hazijathibitishwa.
Shambulio la siku ya Ijumaa limefanyika takriban saa 5 asubuhi saa za Nigeria, katika eneo la kibalozu, katikati ya Jiji la Lagos, karibu na ubalozi wa Marekani. Kulikuwa na mlipuko mkubwa na moshi kutanda ukitoka ndani ya jengo.
“Niliona miili imetapakaa,” Michael Ofilaje, mfanyakazi wa UNICEF anayefanya kazi katika jengo hilo amesema, kwa mujibu wa shirika la habario la AFP.”Watu wengi wamekufa.” Amesema alihisi kama “mlipuko huo umetokea chini ya jengo na kutikisa jengo zima”. Polisi wamefunga eneo hilo la tukio.
“Tumepeleka polisi wetu na kundi la wataalam wa mabomu. Hatuwezi kusema watu wangapi wamekufa,” amesema msemaji wa polisi wa Abuja, kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press.
-BBC