WATAYARISHAJI wa Festival ya ‘Brüderschaft der völker’ mjini Aschaffenburg,
nchini Ujeruamani, wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonesho hayo ya utamaduni wa nchi mbalimbali yatakayofanyika Julai 19 hadi 21, 2013.
Watayarishaji wa maonesho hayo wamevutiwa sana na shughuli za Umoja wa Watanzania ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania, wandaaji wa onesho hilo wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.
Mwenyekiti wa UTU, Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi Ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania.
Umoja wa Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.
Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com pia unaweza kutembelea link ya maonyesho at http://www.bruederschaft-der-voelker.de/2013/05/29/union-of-tanzanians-in-germany/