Mwenyekiti wa Umoja wa wapanda pikipiki wa mkoa wa Mwanza Makoye Bunoro (kushoto) akimweleza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi jinsi wapanda pikipiki wanavyohitaji kupata mafunzo na mikopo ya kununua pikipiki kutoka Serikalini ili waweze kujiajiri wenyewe na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Mdhibiti wa mali za chama cha Umoja wa wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza Faraji Abdalah (kushoto) akimwelezea Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) jinsi umoja huo ulivyoweza kuunda kitengo cha polisi jamii ambacho kinashirikiana na Jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.